Uzalo Special Thread

[emoji23][emoji23][emoji23]niachie mafia wangu Zulu
Pambana na mume mwenzio Ayanda
We panya road bwege sanΓ  ngoja nimwambie mangcobo pale kwake πŸ˜‚πŸ˜‚

Ila kuna matacle mawili yananipa mzuka.
Kuna la mamlahmbo, alafu kuna mke mwenzio mangcobo nyieee,
Nakonda moyo
 
Hivi sma alishawaambia ayanda na manzuza kuhusu hiyo mimba feki au?

Maana manzuza kwa kupanick sijui mlokole gani yule?πŸ˜‚
nadhani bado... me enyewe nasubiri hicho kizungumkuti kwa huyo mama wa mapanic na uyo mtoto wake ayanda sjui watamchukuliaje sma
 
Thanks dear
 
mmmmh, incase hujaangalia ya leo fanya kesho saa tatu na nusu asubuhi uangalie marudio[emoji20]
 
Hii leo ni tuseme kwikwi ama nini daah ni moja ya scene za moto sanaaa.

Ok
Amos alikuja kumchukua sba na kumtoa out na dhlomo akawapa baraka zote kisha kuwaruhusu,

Akiwa kazini dhlomo akiongea na mondil ,anapewa file la kesi ya mtu mmoja na mondil, jamaa anamuomba dhlomo wasaidiane waweze kumaliza kwani amepokea simu kutoka kituo cha polisi hillbrow joburg kuwa jamaa huyo (amos) ameonekana huku durban na amekuwa akijihusisha na human trafficking na prostitution ,

Dhlomo anaanza kukandia kuwa wasichana wenyewe ndio chanzo kwani wakisikia tu joburg wanaweweseka na kutaka kwenda haraka kwahiyo acha wauzwe tu..

Lakini anapolitazama file anakutana na picha ya amos hapo dhlomo anapatwa na muhaho sana na kumpigia polisi mmoja ambaye yupo patrol anaitwa nyawo kuwa afuatilie nyendo na kumpa namba ya gari wakiloondoka nalo na number..

Huko kwa mangcobo nosi akiwa na mama yake wanampigia mabuza anakuja na anauliza mbona usiku usiku sana kulikoni?

Anaambiwa kuwa nosi amekubali kwenda tena kwa pravesh usiku huu hivyo atarecord tena..

Nosi anasisitiza kuwa ingekuwa mxo lazima angefanya kwa ajili yake so naye lazima amsaidie kwa hili. Mabuza anapongeza na kuondoka zake..

Dhlomo akiwa bado kituoni pale counter anahangaika ,anatokea sergeant mdunge na kumwambia mbona bado yupo hapo mpaka sasa? Alidhani dhlomo atakusa kwenye sofa home akicheki pastor akiwa live kideoni, dhlomo anacheka tu kwa kujilazimisha kidogo

Jamaa huyo (mdunge) anaendelea kupiga story zake na kudai kuwa asingekuwa na shift ya usiku basi angeenda home lakini anatumiwa updates na demu wake kupitia WhatsApp. Dhlomo anazuga zuga Kisha anapigiwa simu na nyawo kupewa updates halafu anasepa fasta kumfata sibahle ..

Nosi anaenda kukutana na pravesh kisha wanaagiza shots mbili mbili na kunywa huku nosi akiahidi kumpa uroda pravesh mpaka ajishike kisogo,πŸ˜‚

Wanazama zao room kupeana ile kitu inamesa mwensake.

Kule jela mxo na zweli wamebanwa chemba na kundi la mindlos na mwenyewe akiwemo pia , wanaomba msamaha ila mindlos ana hasira na kudai mxo anajifanya gangwe mpaka huku jela wakati hapo mindlos yeye ndo big boss.

Zweli anadakia kuomba msamaha lakini jamaa linasema anyamaze lina kesi na mxo zaidi, muda huo kina wamebanwa mikono nyuma na wahuni hao.

Mindlos anafoka kuwa mxo licha ya kumchoma polisi bado ameamua kufanya uhuni ili yeye (mindlos) ahamishwe ..!

Mxo anajutia na kudai hatomsumbua tena mindlos lakini jamaa linadai leo watakiona kilichomtoa kanga manyoya πŸ˜‚

Wanaanza kula kibano sanaa

Kule kanisani pastor anafanya mafekeche yake kama kawaida kitu kiko live kwenye kideo .

Dhlomo anaenda mpaka kule alikopewa direction ndani ya gari lake nje anamuona mwanaye akiwa kashikwa kiuno na njemba nene na ndevu kama mswalisuna πŸ˜‚
Pembeni yuko amos akisisitiza njemba ile ilipe pesa kwanza na jamaa linafunguka misimbazi kibwena pale kishs linamkiss sibahle hapo amos akisifia kuwa pisi kali hiyo..
Dhlomo anashuka na kumfata sibahle anamvuta mkono na lile njemba linamshika kws nguvu sba, halafu linamkiss tena ,hapo dhlomo anaishiwa nguvu kisha taratibu anageuzs zake na kusepa akimwacha sba njiapanda..πŸ˜₯πŸ˜₯

Kanisani pastor anaangusha watu feki pale huku nyuma kukiwa na projector ikioneshs kilichomo mbele mara ayanda anafika na ile camera akiwa na gc na thobi kisha Fasta anatoa waya wa vga uliotungwa na kuchomeka kwenye camera ile wsliyoiba kws nkosi.

Mara mbele ukutani inajioneshs ile clip ya pastor na fikile wakipigana makiss pale kitini na hakafu inafatia ile ya yule jamaa aliyekuja kudai hela alijifanyaga kilema.

Pastor anapigwa butwaa na kudai waumini wasimsikilize gc ni mzushi ,hapo gc anaanza kuelezea wslivyotapeliwa pesa na pastor na ayanda anasogea mbele haoo nkosi anachomoka na kurusha ngumi mkono alioshika fimbo ili ampige ayanda lakini muhuni anakwepa na kumjaza pastor moja ya uso mpaka chali mithili ya gunia la viazi.

Kisha ayanda anakaa juu ya pastor na kuanza kumpa vitasa vya hela yote..

Kule jela kina mxo na zweli wsmechakaa kwa kipigo na uso hautamaniki kabisa .
Mindlos anasema mxo auwawe hapo hapo na zweli aachwe ili akasimulie huko uraiani ,mxo anadai ana hela walizompora zakes atampa zote lakini jamaa linagoma na kudai atatuamiaje akiwa jela? Kisha linaamuru mfungwa mmoja ammalize mxo kisha jamaa anachomoa kisu na kumkita nacho mxo tumboni halafu wanapotea zao na kumuacha zweli akiwa anamlilia mxo na kupiga kelele kuomba msaada.
Mondil akiwa home anaona kideoni ngumi za nkosi na ayanda anampigia jirani yake na kumuomba amuangalize mtoto wake hapo kisha anaenda kanisani..

Muda huo kanisani ayanda anaamka huku akiwa na wenge waumini wote wanamuangalia yeye tu kwanini kafanya vile, nyuma yake nkosi anaamka na kurusha tena ngumi na gc anamshtua ayanda na ayanda anakwepa na kumpiga ngumi pastor anajigonga kwenye kingo ya kiti pale anazima kimya, ayanda anapatwa na muhaho sana snajua ameuwa anaanza kumuamsha nkosi lakini kimya .

Huku kule jela zweli akilia kumuamsha mxo aliyetulia chini.

Nosi kule hotelini anamdadisi pravesh na jamaa anafubguka kuwa mkewe nerina alicheat na mdogo wake (pravesh) na dogo lake akakimbilia india hivyo akamfungia mkewe ndani ili akili yake ijirudi maana naye mkewe alitaka kukimbilia india pia.

So anadai haikuwa nia yake kumuuwa ila upinzani alioleta mkewe ndo ulikuwa shida hivyo akammaliza na mwili kuutelekeza beach nyuma ya boot la gari.

Anamsihi nosi asiseme nosi anaahidi kukaa kimya kisha anaaga kwenda uwani ila katika purukushani zao mkoba unaanguka na kile kitape kinadondoka jamaa anaokota na kuuliza cha nini,

Nosi anajibu huwa wsnatumia kurekodia kwaya kanisani, jamaa anaomba wasikilize aone, hapo kila alichoongea kinasikika ,anapanick na kumkaba nosi kisha kumtupa kitandani huku akiuliza nosi ni nani?

Pale jela anafika afande na kupiga simu kuws mxo na zweli wanahitaji msaada haraka .

NB: maji na mafuta yameanza kujichuja,sasa malaya ni malaya janbjam ni jambazi.

Nosi, ayanda hawaamini macho yao..
Jagiya Vera ginger MAFIA cartel
Na wengineo.

Post hii kwa wale ambao waliikosa wote twendeni hapa..
 
Daah mxo jembe langu huyu afande nimehamisha moyo simtaki tena shenzy zake.

Sba namuonea huruma sana yuko na mtihani mzito.

Ayanda akamatwe sababu naye amemjeruhi mtu pia .
Nosi nadhani ndo anakufa hivyo maana niliskia hana muda mrefu hapo kwa mashu

Daah nosi wangu tumuombee uzima huenda ni tetesi tu
 
Nosi mbona niliona kuna pic kapiga na baba ake mdogo
 
So pastor kafa?
 
Nosi mbona niliona kuna pic kapiga na baba ake mdogo
Nadhani ni hapa kwenye tamthilia tu .
Lakini tusubiri mimi naombea aendelee kubaki labda atapona halafu wakati jamaa linamkaba ile tape ikiendelea kurecord tu.
 
Wee panyarodi Jagiya ndo kusema unamliwaza mzee baba yule na stress za mwanaye kufanywa mtaji?πŸ˜‚
 
Pia tuacheni tabia ya ubinafsi .
Mtu kama umeangalia ni vema ukaweka updates hata kidogo kwa ambao wamekosa wakapata hints kidogo kuliko kukaa kimya wengine wapo safari wengine mikoani huko..
Kama ambavyo huyu dada nanii huyuu, na jagiya huwa wanafanya na mimi pia .

Tchao

Tupendane
 
Mambo yalikua fayaaa leo kwa mashu yaan n balaaa
Nosi yupo sanaa tu bado usife moyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…