Uzalo Special Thread

Yeah kwakweli maana sio kila mda mtu anaweza bahatika kuona so inakua msaada tosha
 
Zakhie the mafian,nilipenda commitments ya huyu jamaa,Richa ya kukaa jera muda mrefu,jamaa alikuwa na roho ngumu sana,
I love you my Lili [emoji23][emoji23] noma sana
 
Umeupiga mwingi sana thanks for the update
 
Nimeangalia marudio ya wiki nzima baadhi Its Pancho ashayaelezea Mimi ntamalizia mengine


Nosipho alifanikiwa kumtoroka pravesh na kuondoka na ushahidi kwenye tape

Pastor Nkosi amekufa ana Ayanda ndo mtuhumiwa amakamatwa na yuko kituoni kusubiria hukumu

Gerezani Mxolisi alichomwa kisu na watu wa Mindlos lakini ana bahati askari magereza ambulance na kuwahishwa hospitali


Dholomo baada ya kujua Sibahle ni prostitute anamlia buyu hamuongeleshi japokua sibahle anajaribu kuomba msamaha


Mabuza baada ya kupewa ushahidi na nosipho anatokomea na hapatikani kwenye simu


Ayanda akiwa Gerezani hajui la kufanya Ghafla mangconbo akiwa hospitali kumuona Mxolisi ambaye amechomwa kisu anaona taarifa Kwenye gazeti kwamba Ayanda ameua hivyo anawahi kituoni na mwanasheria (Shaun) kumsaidia mwanae Ayanda


Mangcobo baada ya kumkabidhi Shaun kwa Ayanda ili apewe muongozo anatoka nje na kukutana na Manzuza halafu Manzuza anaanza kumlaumu Mangcobo kwa kuharibu future ya watoto wake na awaache na familia yake


Mangcobo anamchana Manzuza kwamba anadai wale watoto ni wake lakini hamna chochote anachofanya zaidi ya ku judge na Mangocobo anamuuliza Manzuza we umefanya nini zaidi ya kusali kisha Mangcobo anasema wewe endelea kusali wakati Mimi nahangaika Ayanda asifungwe endelea kusali wakati nahakikisha Mxolisi anapona hospitali halafu baadae uwaambie ulikua unasali


Maneno yalimuingia Manzuza mpaka akakaa kimya Baada ya hapo Manzuza anaenda hospital anamkuta Mangcobo akiwa na Mxolisi anashikwa na aibu kisha wanashikana mikono na wanamuombea Mxolisi


Mxolisi anazinduka baada ya maombi kufanya kazi



Mabuza anaenda hospitali kumuona mxolisi na kumwambia ushahidi anao lakini anataka 1 million Rand ndo atoe ushahidi ule wa kwenye tape


Kanisa halina hela limefilisika Pastor Nkosi katumbua hela zotee hivo wanamuomba Mamlambo awasaidie kufufua kanisa


Kuna Mshkaji anamlia mingo Gc naona ameelewa mzigo
 
Dhlomo anaenda hospital kumuona Mxolisi na kumwambia muda wa kukaa hospitali umeisha anatakiwa arudi jela

Mxolisi anajitetea kwamba bado anaumwa anahitaji muda apone na kule jela sio pazuri maana mindlos anataka kumuua

Dhlomo anamwambia Mimi sijali kama kuna mtu anataka kukuua ila jela lazima urudi


Mxolisi anachonga na daktari ili aongezewe muda wa kukaa hospitali na atampa hela daktari anakubali kumuongezea wiki moja hospitali


Ayanda ametoka kituoni kwa dhamana lakini hafurahii anajiona mwenye hatia kwakua ameua


Mengine nimesahau......
 
Big up mkuu@Its Pancho
 
Hakuna briefing kidogo kwa aliyecheki leo?
Nilifurahi huyu mkuda kutolewa kwenye kesi..
 
Naomba nifahamishwe marudio huwa ni lini na lini na muda!
Marudio ni jumatatu hadi ijumaa saa tatu na nusu asubuhi na jumapili ni marudio ya wiki nzima kuanzia saa nne (sina hakika sana kwa anaefahamu anirekebishe muda)
 
How can a man waste his time to watch this kind of Tv show everyday from Monday to Friday at 1930 instead of that time to be at bar drinking beers with friends or at club.
 
Naona kule uzaloni ameingia kiumbe mpya yule aliyekuwa muuza bar katili wa Isidingo. Halafu Mxo kajigonga. Hapo wamekutana wapiga dili wawili. Mbaya zaidi kaja na gari kali vijana wameshaanza kujadili bei yake. Halafu Ayanda baada ya kumuona Sbha baona amechanganyikiwa hata Sma hamuelewi. Twende mdomdogo.
 
How can a man waste his time to watch this kind of Tv show everyday from Monday to Friday at 1930 instead of that time to be at bar drinking beers with friends or at club.
Uzalo ina dakika 22 tu, rudia tena hiyo 22,
Halafu ina uhalisia, tofauti sana na mi tamthilia watu wanayoangalia siku hizi

Watu wanaangalia mi tamthilia episode moja dakika 45 ama zaidi ya saa moja, tena wanabeba season nzima wanakesha wanatazama.

Uzalo, unaitazama saa moja na nusu hadi saa mbili unatazama habari, rudia tena kusoma ukimaliza kuangalia uzalo unatazama taarifa ya habari, sasa hiyo beer na mabar ya nini??!! Huko ni Kutafuta hangover siku za kazi Monday to Friday, bia wengi hunywa wikendi,
 
How can a man waste his time to watch this kind of Tv show everyday from Monday to Friday at 1930 instead of that time to be at bar drinking beers with friends or at club.
Mimi nimeachana na mapombe kabisa.Tamthilia kama Uzalo ni baadhi ya vitu vinavyonisaidia katika hilo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…