Uzalo Special Thread

Safi sana ninachoona hapo ni kuwa mxo bado ana muda mrefu kuishi uraiani.
Tena nataka amle na sba kanisa ayanda arudi kwa mkewe wakapeane mimba feki..

Akijaribu kumpa nazi sma ndio atauona moto wa zweli.

Sasa huyu sba kisa cha kupeleka umbea mwenzie aachike au?
 
Safi sana mkuu.. sipati picha ayanda atakavyokwenda kwa smangele huku akijua ile siyo mimbaa... aisee atamkata makofiii ya hatarii
Sidhani kama ataamini,maana alishuhudia kwenye upimaji tumbo na mtoto kwenye utrasound
 
Safi sana mkuu.. sipati picha ayanda atakavyokwenda kwa smangele huku akijua ile siyo mimbaa... aisee atamkata makofiii ya hatarii
apo ndio patam... tena patam haswaa
 
Hahaaa sba anampenda sana ayanda tena alivyojua uongo wa sma alifurah mbaya maaana ameona ayanda anaenda kuwa wake mazma
Natamani bifu la mxo na la ayanda lianze upya (bifu la kugombea pisi kalii) 😁
 
Ivi jamani ukiingia kwenye website ya itv unaweza kuangalia vipindi kama kawaida
 
Hahaaa sba anampenda sana ayanda tena alivyojua uongo wa sma alifurah mbaya maaana ameona ayanda anaenda kuwa wake mazma
Natamani bifu la mxo na la ayanda lianze upya (bifu la kugombea pisi kalii) 😁
Vyovyote itakavyokuwa i stand with mxo 😂
 
Ayanda akiwa chumbani na smangele,anamlazimisha apandishe pajama aliyovaa ili mradi ashuhudie kama ana mimba ya kweli au ya uwongo hii ni baada ya kuambiwa na sibahle kwamba mke wako anakudanganya

So smangele atachukia baada ya kuambiwa apandishe pajama na kuondoka chumbani kuelekea sebuleni ambapo yupo manzuza na aunt yake Ayanda
So wakina manzuza watauliza kulikoni ,Ayanda atasema nilikuwa nataka kujua kama mimba ya sma kama ya uongo au ya ukweli ,Kisha sma atadakia na kubadilisha mada kwamba ugomvi wetu si kuhusu mimba Bali ni ishu ya Ayanda kutembea na wanawake wengine lakini aunt atamuuliza sma mbona sasa kama mimba yako ni ya ukweli
Mbona mtoto asikiki akipiga mateke
Sma ataishia kujibu tu kwamba mtoto huwa anapiga mateke akijisikia.


Baada ya mangcobo na mxolisi kugundua kwamba mondli amefahamu kuhusu mauaji ya nkosinathi,wanaamua kuutoa mwili wa nkosinathi kwenye ofisi ya panel beater na kuufukia sehemu Kisha wanashauriana kuhusu kumtumia sms manzuza kumjulisha sehemu ulipo mwili wa mtoto wake marehemu .


Nosipho akiwa njiani anatembea anakutana na mondli ,Kisha mondli anaomba kuongea nae kwa muda kuhusu mambo mabaya waliofanya mama na kaka ake ,lakini nosipho anakataa kata kata na kuwatetea lakini mondli anamwambia utapata kujua ukweli hivi karibuni.


Baada ya manzuza kupata ujumbe wa sehemu alipozikwa nkosinathi ,anamtaarifu mondli ambaye mara moja anaanza shughuli ya kwenda eneo la tukio na kufukua
Baada ya kufukua mabaki ya mwili yanaenda kupimwa vinasaba na kujulikana kwamba ni ya nkosinathi
So baada ya hapo manzuza analia sana


Nosipho akiwa nyumbani anamface mama ake na kumuuliza kuhusu kuusika kwake kwenye mauaji ya nkosinathi ,lakini kabla ya hajajibu anamwambia nilikuwa nahisi tangu muda tu kwamba nyie ni mashetani wewe na mxolisi na ndio maana ulikuwa unamwota sana usiku nkosinathi,Kisha baada ya hapo nosipho anaondoka akiwa analia.



Nosipho anaelekea kwa mondli na kumwambia amsamehe kwa kutokumwamini kwa maana ameshawajua wauaji wa nkosinathi ghafla wakiwa wanaendelea na maongezi anatokea mama ake bandile ,so nosipho anashangaa kumwona pale na machozi yanamtoka na anaamua kumwambia mondli mbona ulikuwa unanidanganya kwamba hujui alipo kumbe upo nae humu ndani kabla mondli ajajibu nosipho anaondoka akiwa bado analia.
 
Yeah ugonjwa huo umepunguza ngozi yake nzuri kwa kiasi kikubwa.
Lakini bado ni mrembo sana mkuu

UFAHAMU UGONJWA WA VITILIGO
Vitiligo ni ugonjwa ambao unaathiri ngozi,unaotokana na kuharibiwa kwa cells za kutengeneza rangi ya ngozi zinazojulikana kama (melanocytes). Chanzo halisi cha celi hizi kushambuliwa bado hakijajulikana kitaalam, hivyo Wataalam Wengi kupata ugumu wa kujua tiba sahihi ya ugonjwa huu.Tatizo hili la ugonjwa wa ngozi kwa anaye hitaji dawa za kienyeji ambazo zina uwezo wa kutibu na kuondoa kabisa ugonjwa huu hatari wasiliana nami kwa +255766950256
 
Asante kwa update mkuu
 
Umetisha sanaaaa
 
Sijaangalia uzalo muda mrefu tokea siku ile ayanda anamtafuta smangele alivyopotea ghafla akawa haonekani nyumban na ayanda akawa hajui alipo.. zishapita kama week 3 sasa.. mwenye update yeyote naomba anijuze.. vip smangele alifanikiwa kuunganisha mimba feki kwa mumewe na kupata mtoto wa kununua..? Vip sakat la mondil na wale shemej zake walioua mtu limefikia wapi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…