kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
"Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la watu"
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la watu ambalo linatarajiwa kufikia milioni 90 mwaka 2050.
Akizindua ripoti ya idadi ya watu katika ngazi ya taifa, wilaya, kata na shehia, jana jijini Dar es Salaam, Pinda alisema ni vyema kuzingatia uzazi wa mpango kama ilivyoainishwa katika sera ya watu ya mwaka 2006.
"Sera ya idadi ya watu inatutaka tuzae watoto ambao tunaweza kuwahudumia katika maendeleo yao ya baadaye na Taifa kwa jumla," alisema Waziri Mkuu Pinda.
Alisema ni vyema Watanzania wakaachana na dhana potofu kuwa kuzaa watoto wengi ni umaarufu nautajiri. Desemba 31, mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete alizindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2012 ambapo idadi ya Watanzania ilifikia milioni 44.9.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa wanawake ni asilimia 51 wakati wanaume ni asilimia 49. Kimkoa, ripoti hiyo ilionyesha mikoayenye idadi kubwa ya watu kuwa ni Dar es Salaam wenye idadi ya watu 4,364,541. Mwanza 2, 727, 509 na Mbeya 2,707,410.
Pinda alisema, Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhimiza matumizi ya uzazi wa mpango kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la idadi ya watu. Vilevile Pinda alisema iwapo ongezeko la watu la asilimia 2.7 kwa mwaka litaendelea basi idadi ya watu Tanzania itafikia milioni 90 ifikapo mwaka 2050.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una ongezeko kubwa la watu kwa asilimia 5.6 kwa mwaka ukifuatiwa na Mkoa wa Mjini Magharibi na Unguja ambapo kasi katika miji hiyo ni asilimia 4.2.
"Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu jijini Dar es Salaam ni kubwa sana. Kwa maana hiyo asilimia 10 ya Watanzania wanaishi Dar," alisema.
Alisema msongamano wa watu katika miji hiyo ni mkubwa na unasababisha shinikizo katika utoaji wa huduma za maendeleo kama maji, elimu, afya, umeme na miundombinu.
Chanzo: Mwananchi