Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

"Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la watu"
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la watu ambalo linatarajiwa kufikia milioni 90 mwaka 2050.

Akizindua ripoti ya idadi ya watu katika ngazi ya taifa, wilaya, kata na shehia, jana jijini Dar es Salaam, Pinda alisema ni vyema kuzingatia uzazi wa mpango kama ilivyoainishwa katika sera ya watu ya mwaka 2006.

"Sera ya idadi ya watu inatutaka tuzae watoto ambao tunaweza kuwahudumia katika maendeleo yao ya baadaye na Taifa kwa jumla," alisema Waziri Mkuu Pinda.

Alisema ni vyema Watanzania wakaachana na dhana potofu kuwa kuzaa watoto wengi ni umaarufu nautajiri. Desemba 31, mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete alizindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2012 ambapo idadi ya Watanzania ilifikia milioni 44.9.

Matokeo hayo yalionyesha kuwa wanawake ni asilimia 51 wakati wanaume ni asilimia 49. Kimkoa, ripoti hiyo ilionyesha mikoayenye idadi kubwa ya watu kuwa ni Dar es Salaam wenye idadi ya watu 4,364,541. Mwanza 2, 727, 509 na Mbeya 2,707,410.

Pinda alisema, Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi kuhimiza matumizi ya uzazi wa mpango kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la idadi ya watu. Vilevile Pinda alisema iwapo ongezeko la watu la asilimia 2.7 kwa mwaka litaendelea basi idadi ya watu Tanzania itafikia milioni 90 ifikapo mwaka 2050.

Ripoti hiyo ilionyesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una ongezeko kubwa la watu kwa asilimia 5.6 kwa mwaka ukifuatiwa na Mkoa wa Mjini Magharibi na Unguja ambapo kasi katika miji hiyo ni asilimia 4.2.
"Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu jijini Dar es Salaam ni kubwa sana. Kwa maana hiyo asilimia 10 ya Watanzania wanaishi Dar," alisema.

Alisema msongamano wa watu katika miji hiyo ni mkubwa na unasababisha shinikizo katika utoaji wa huduma za maendeleo kama maji, elimu, afya, umeme na miundombinu.

Chanzo: Mwananchi
 
Wanajamvi habari,

Naomba tuwekane sawa na kupeana uzoefu kwa hili. Hivi ni sahihi mwanamke kutumia uzazi wa mpango(eg. sindano) bila mumewe kufahamu?

Nimelipata hili kwa swahiba wangu hapa ofisini.

Ameniomba nimshauri kwani amegundua mkewe anatumia uzazi wa mpango kwa siri.
 
mijanaume mingine mibishi unaweza kujikuta mwaka mimba mwaka mtoto hajali kuhusu afya yako wala usalama wako na watoto yeye anajua kuongeza ukoo wake tu...hapo kimya kimya unapiga sindano zako unatulia
 
Ni vizuri kushirikishana, ili mume awe aware na iko ki2, lakn wanaume wengne wabishi na hawatak ata kuckia habar za uzaz wa mpango.. Muulize kwanza uyo swahiba wako yeye alishawah kumwambia mkewe kuwa hataki njia za uzaz wa mpango!? Kma ndio basi uyo mke ana haki ya kufanya siri, kama hapana there is something behind the scene!
 
Hivi ukishaanza period si ndiyo yai limeshavunjika hivyo huwezishika ujauzito tena? au nimesahau kidogo. By the way hivyo vidonge inasemekana vina madhara kibao mwilini.
 
Kazi ya vidonge vya uzazi wa mpango ni kujenga mazingira ambapo yai halipevuki.Wakati wowote unapoanza kuvitumia unapata kinga kuazia hapo.Wanashauri uanze kutumia siku ya kuanza ya period ili kuepuka ku-enterfere mzuguko(cycle) yako ya mwezi,lakini haina maana kwamba ukianzia hata katikati ya cycle au baada ya hizo siku 3 haitafanya kazi.

Lakini pia ni kweli kwamba ukiona period ina maana kwamba hujashika mimba lkn it's not always true. Kwa sababu si kila bleed ni period na pia kuna uwezekano wa kushika mimba lkn bado ukaona periods zako kwa miezi hata mitatu ya mwazo.
 
Kama unaweza zile siku bora utumie hizo maana kwa uchunguzi mdogo tuu wa bibie wangu hivi vidonge vinamfanye akose hamu ya tendo kama awali hata yeye anashangaa kwa hyo siku hizi tunahesabu tuu ikiwa danger day tunatulia
 
anomba nielezwe kuhusu pharmacokinetics za hiyo dawa Dosage,route of administration, where is it distributed in the body, where and how is it metabolised, how and where is it eliminated,half life yake ngapi? contraindications,teratogenecity? any drug intraction? antidote in case of poisoning? side effects? therapeutic window and therapeutic index?, volume of distribution? inatarget receptor zipi? bioavailability yake? does it bind to plasma?

dawa za hospitalini zimetengenezwa na kujaribiwa kitaalam. najua ni imani potofu ya wengi kua dawa za hospital zina madhara na za kienyeji ndo salama

Take care!!!:A S-key:
 
Mbona masharti ya kishirikina?
Kuna haja gani ya kufukia sufuria na dawa chini ya ardhi wakati dawa umeshakunywa?

Napenda kujua What does the dawa do to the body that brings about kutikuzaa(mechanism of action)? Manake madhara mengi ya madawa ya uzazi wa mpango yanatokana their actions.
 
Habarini za asubuhi waungwana,.
Kwanza napenda kuwapa pole na shughuli na mihangaiko ya siku, naomba msaada wa ushauri nipo katika wakati mgumu sana. Mke wangu amejifungua mtoto mwaka jana mwezi wa sita, sasa hv mtoto wetu huyu wa pili ana mwaka mmoja na miezi 2.
Kwa kipindi chote tangu alipojifungua tumekuwa tukitumia njia ya uzazi wa mpango kwa kutumia vidonge vya majira, sasa mwezi wa saba mwaka huu tulishauriana abadili njia nyingine kutokana na hali aliyokuwa anajisikia iliyokuwa inasababishwa na vidonge. Tuliamua kutumia njia ya sindano, alikwenda hospitali ya Wilaya wakampa hiyo huduma. sasa mwezi huo wa saba umepita bila kuona siku zake.Jana baada ya kuona muda umepita sana akaamua kwenda kupima ujauzito, majibu yakawa yupo Positive. sasa naomba ushauri wenu ikiachwa hii haiwezi kuwa na madhara kwa mtoto ambaye bado ananyonya? Msada nini kifanyike.
 
Dah! Kweli majanga! ngoja wenye watoto zao waje loh!
 
Ndio imeshatokea hivyo, inabidi mkubali hali halisi.

Leeni mimba na dogo ale vizuri maisha yaendelee. Sidhani kama kuna madhara yoyote yale zaidi ya kuangalia afya ya mama iwapo mara ya mwisho alijifungua kwa operesheni.
 
pole sana mkuu,ilitakiwa alipoanza kutumia sindano awe anatumia na njia nyingine kama condom kwa muda wa kama wiki 4-6 za mwanzo,pole sana kwa kutoambiwa hili wakati mkeo alipoanzishiwa sindano.
Kwa sababu mimba imeshaingia, muendelee tu kulea huo ujauzito,japokuwa itamchisha mama lakini thats the best option for now.
 
Mi wasiwasi wangu ni madhara ambayo hiyo mimba aliyonayo inaweza pata kutokana na sumu ya hiyo sindano aliyokwishachoma. Kwani ni sindano ya kuzuia Kwa muda gani alichoma.
 
Ila wanasema njia ya kienyeji isiyo na madhara yeyote ni, bibie anywe maji ya baridi kama lita moja then anawe vizuri tuu kwa bibi.
 
Kabla ya kuchangia chochote ngoja nikushangae kwanza....ila kweli kuna mabest mnajua kupotea lol...karibu tena best!!

Ndio imeshatokea hivyo, inabidi mkubali hali halisi.

Leeni mimba na dogo ale vizuri maisha yaendelee. Sidhani kama kuna madhara yoyote yale zaidi ya kuangalia afya ya mama iwapo mara ya mwisho alijifungua kwa operesheni.
 
Kabla ya kuchangia chochote ngoja nikushangae kwanza....ila kweli kuna mabest mnajua kupotea lol...karibu tena best!!

Hehehehe asante besti. . .nilikuwa napalilia palilia mazao. Changia basi alafu tukashangaane chiti chati.
 
Back
Top Bottom