Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Kusema ukweli hili somo ni zuri sana!! Kuliko kuchoropoa viumbe wasio na hatia, kuvuruga mipango yako kwa mimba zisizotarajiwa(especially wanafunzi na wale wasiojiweza kulea ambao wengi wao huishia kutupa au kutelekeza watoto), ni bora kabisa kuchukua hatua stahiki mapema! Wimbo wa ku-abstain umeshakua sugu hata kwa hawa vijana wadogo, elimu kama hii itasaidia walau kupunguza matokeo hasi yaletwayo na mimba zisizotarajiwa. Asante sana afrodenzi, mi mependa iyo heading pia..........imebeba ujumbe mzito na wa maana sana!!!! Stay blessed dear....

Kipipi
Kabisa mamake asante sana kwa majibu yako
Kwa kweli umenena chaa maana sana dear .
 
Haya bana ladies,sie vidume tunacheki mchezo tu!Lakin wengine mashuti yetu yanachanaga nyavu!

Ku cheki tu haitoshi dear.
kusaidia na kutoa mawili matatu inaweza msaidia
hata yule visitor tu . asante ...
 
Mkuu, umezungumzia point nzuru sana.

1. Huko mashuleni ndio balaa zaidi, walimu kama wanaeleza hii ni kwa juu juu tu kwani wakisema kwa undani (wengine) watakuwa wanafunga milango yao. Tukumbuke walimu ni sehemu kubwa ya wanaofanya mapenzi na wanafunzi.

2. Ama kwa kuona haya, au bado kuliona tendo la ngono ni taboo, wazazi wengi hawawaelezi watoto wao juu ya hizi hatari. Kama elimu ingekuwa inatolewa kwa wazazi na watu wa karibu kwanza, pengine hili tatizo lisingekuwa kubwa kiasi hiki. Kitu cha ajabu, wazazi wanashindwa kumweleza mtoto madhara ya ngono zembe lakini wanawafunda jinsi ya kumridhisha mume. Mafunzo yale wasichana wanayatumia kuwafurahisha wanaume kabla ya waume.

3. Tatizo la tatu ambalo ndio kikwazo kikubwa kwa elimu ya ngono ni shinikizo la dini. Watu wa dini wanajua tu kusema njia za kuzuwia mimba ni haramu (mkazo mkubwa ukiwa kwa matumizi ya kondom ambayo ndio salama na isiyoleta usumbufu wowote kwa watumiaji zaidi ya ulafi wao wa kutaka kutwanga kavukavu.

Ni kweli Mkuu, bado tuna safari ndefu sana.

Ukweli mtupu. asante mkuu
 
Hiyo point ya kwanza umenikumbusha wakati mwalimu anatufundisha Biology mambo mengine alikuwa anafunika anayapitia juu juu sasa sijui alikuwa anaona soo au vipi na bado hali hii inaendelea kuwepo kwenye shule nyingi tu hapa bongo

dahhh kama mwalimu anaona soo.. wanafunzi watajifunza vipi?
 
dahhh kama mwalimu anaona soo.. wanafunzi watajifunza vipi?
Sasa ndio hapo mwanafunzi akiishajua inakuwa too late na mambo yanakuwa yameishaharibika....halafu yaani wewe nitakulaza kwenye mapipa kabisa hebu njoo kule kwanza la si hivyo leo ni viboko kabisa tena namwambia Lizzy akachume mpera kabisa..
 
Sasa ndio hapo mwanafunzi akiishajua inakuwa too late na mambo yanakuwa yameishaharibika....halafu yaani wewe nitakulaza kwenye mapipa kabisa hebu njoo kule kwanza la si hivyo leo ni viboko kabisa tena namwambia Lizzy akachume mpera kabisa..

Yawiiii.
yeah nakumbuka kipindi kile niko msingi.
Ukisikia neno chupi unadhani mtu katuka dahh..
Lakini hii inbadilika taaratibu sasa .

Lakini usema ukweli hii elemu ya kuzuia mimba ni muhimu sana
tunatakiwa tuifanyie kazi kwa kweli kwa wanafunzi, nawale ambao
hawako tayari. mi mambo ya kutoa mimba sijui kutupa watoto yanani
chefua kwa kweli..
 
Uzi umzuri sana ila tatizo lake bana haya madude yanayoitwa condom mhhh ni balaa lake ukikutana nayo ni issue nyingine

AD ukumbuke kuwa wako wanawake wengi sana wanaolalamika sana hukusu hizi njia za kuzuia mimba
Wengine zinawaletea allergy na wengine wanalalamika sana maumivu ya tumbo
So kwa hizi njia wengi wako tayari sana kutumia condom kama wawili wanaopendana watakubaliana kutumia hiyo ambayo ndio njia moja rahisi sana na isiyotumia muda mrefu
Ila hizo za pills na constraceptive kwa wengi zina matatizo madogo madogo ambayo kwa wanawake yanawakazwa sana kuzitumia
 
uzi umzuri sana ila tatizo lake bana haya madude yanayoitwa condom mhhh ni balaa lake ukikutana nayo ni issue nyingine
mmmh utakufa mkuumimi siwezi kumshauti msichana njia nyingine zaidi ya condom just imagine vibinti vinatumia mavidonge masindano ,sijui vitanzi jamani mida hii nooo watu watumie kondomu loh watakwepa na ukimwi pia
 
mmmh utakufa mkuumimi siwezi kumshauti msichana njia nyingine zaidi ya condom just imagine vibinti vinatumia mavidonge masindano ,sijui vitanzi jamani mida hii nooo watu watumie kondomu loh watakwepa na ukimwi pia

Smile asante sana
hapo juu nimeongeza na jingine kuhusu matumizi ya pills na hayo madude mengine na kusema kuwa wapo wengi wanaoyatumia yanawaletea matatizo
Na kwa wasichana ambao wanakua sijui kama kweli hayo madude ni safe sana kwao japo mimi sio doctor ila ni bora kutumia njia nyepesi ambayo haitakuletea madhara huko badaae
 
Hizo njia za uzazi wa mpango kweli ni noma, zinawaletea wadada/wamama shida baadaye, ni kweli bora kondom unajikinga na vyote (mimba/ukimwi na STIs) lakini hata kalenda ni nzuri kwa waelewa

mmmh msichana eg miaka 18-25 na misindano? Vitanzi? Vidonge? Khaaa kisa nini elimu ipo ipo bwana heri watumie condom tu izo njia zingine siziafiki kabisa
 
Angalieni video.
Nahisi kuwaonesha watoto, wasichana na wavulana video kama hii inaweza kuwapa mwamko na kufikiria mara kumi kabla mtu hajaamua kumpa mimba mschana au msichana kuitoa.
ONYO: YALIYOMO KATIKA PICHA HII HAYAFURAHISHI. IKIWA MOYO WAKO MWEPESI USIANGALIE KABISA!!
Kwa kuwa maandishi yako katika Kispanish, unaweza kusogeza video mpaka dakika 1:24 ili kuepuka maandishi.
 
Last edited by a moderator:
Nahisi kuwaonesha watoto, wasichana na wavulana video kama hii inaweza kuwapa mwamko na kufikiria mara kumi kabla mtu hajaamua kumpa mimba mschana au msichana kuitoa.
ONYO: YALIYOMO KATIKA PICHA HII HAYAFURAHISHI. IKIWA MOYO WAKO MWEPESI USIANGALIE KABISA!!
Kwa kuwa maandishi yako katika Kispanish, unaweza kusogeza video mpaka dakika 1:24 ili kuepuka maandishi.


Gosh, nimechungulia tu kwa sekunde baada ya maandishi nikatoa haraka.

Binafsi kwa upande wanafunzi ningeshauri zile ambazo kwa nia ya kifundisha elimu ya uzazi ambazo hata picha zake ni za michoro zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Good topic...but the effectiness and efficiency ya methods zote ni muhimu kuwekwa wazi as well.....secondly both of them zina side effect .....even condoms pia (sometimez to sam pipo). Thus adequate information kwa kila method tajwa ni muhimu kupatikana na kuzingatiwa na mtumiaji kabla ya kufakamia hizo vitu please.......kujua tatizo ni mwanzo wa ufumbuzi
 
Kujua tatizo ni sehemu ya ufumbuzi wake....but wapewe adequate info kama hiyo alotoa RussianRoulete hapo juu tatizo ni hao watoa huduma yaani wanatoa half cooked....sasa sijui na wao ni lay kama clients wao au la....ila kwa kweli ni bora jamii ielimishwe vya kutosha ili tusife kwa ujinga bali uvivu wa kuchagua.....na utakuwa mwanzo mzuri wa sheria kubana wataokutwa na hatia hiyo ya kuchezea uterus kwa starehe ya kupita
 
Back
Top Bottom