Si kweli. Ulimwengu alianza kumkosoa Mkapa mara alipoanza kufanya madudu, japo alimkampenia sana tu. Humjui Jenerali. Mkapa kwa hasira ndio akampokonya uraia. Hapo Mkapa akawa ameanzisha mchezo mchafu sana, ambapo Magufuli kautumia sana hata kwa mapadre na Maaskofu waliomkosoa.
Kumpokonya mtu uraia, kisa anakukosoa, hasa kama anatokea mikoa ya pembezoni. Ni kweli hilo lilimuumiza sana Ulimwengu, lakini huyu ni mpigania haki, jasiri, tangu utotoni, alipokuwa chuo kikuu walikwenda Msumbiji kusaidia vita ya ukombozi. Ni mtu wa vitendo na anafanya anachoamini. Siyo mchumia tumbo. Tatizo tumezoea wazee wanafiki na wachumia tumbo. Ukiona mtu jasiri unaamini tu ana matatizo. Si mtu wa kawaida