DOKEZO Uzembe wa Hospitali Kuu ya Mkoa Morogoro umesababisha kifo cha Mwanafunzi wa SUA

DOKEZO Uzembe wa Hospitali Kuu ya Mkoa Morogoro umesababisha kifo cha Mwanafunzi wa SUA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Intestinal obstruction is always an emergency case once spotted. Kwa mfano mgonjwa akila kitu na kukitapika muda huohuo ,in projectile vomit hiyo inatosha kuhitimisha
Taratibu mkuu haya mambo Yana wenyewe waachie wewe endelea kufanya Yako.
 
Mama yake hawezi kuumia maana inaonekana kuna shortage ya madaktari na aliyekuwepo alikuwa anawafanyia upasuaji mama wajawazito,dont be judgemental kazini,mjamzito ni first priority
Hospital ya mkoa sio kituo cha afya au hospital ya wilaya
Wapo department wise, hivyo general surgery inajitegemea haingiliani na obs/Gyn, correct me if I'm wrong
Labda kuna ishu ingine lkn hiyo ya kua daktar alikua anafanya operation ya mama sidhani
 
Ina uma sana pole kwa wote kwa msiba.
Tatizo ni mifumo labda Mungu alitaka kumuonesha huyo Daktari kwamba hii ajira ya kuhudumia watu ukiifanya vibaya kwa watu usio wajua pia ipo siku hata wewe yatakukuta.
Vijana wengi walipokuwa wanatafuta ajira wanakuwa wapole wakipata kazi wanatufanyia mambo ya ajabu na kusahau kwamba nao wana ndugu zao wanaoweza kukutana na kadhia kama hiyo kwa mfano mimi kila nikienda hospitali hawa jamaa wanavyokunyanyapaa utadhani wao na familia zao huwa hawaumwi, nikienda Polisi wanavyo nipokea kama vile kutafuta haki ni kosa na ni usumbufu kwao,nikienda Ardhi watumishi wao wamekaa mkao wa kuomba rushwa sijui tatizo ni nini? Mifumo yote hii ili ikae sawa kuna haja ya watu wa haki za binadamu wachukue likizo kidogo watuachie tu deal nao kwanza ala wakishika adabu warudi kutetea haki.
UPUMBAVU na WAPUMBAVU kama huu utaisha lini? Mungu alitaka amuoneshe?????????????????????????????????? ........sometimes its better to remain silent.
 
Intestinal Obstruction aint that life threatening condition unless otherwise with complications.

Kwa scenerio ya hapo juu ni kwamba mgonjwa alikua amewekwa kwenye matibabu ambayo ni non surgical kama kuendelea kufanya Iv resuscitation na monitoring.

Mpaka wanasema anaweza kusubiri that means hakua kwenye first priority
Lazima tukubali kwamba wataaluma tunapata shida sana na mazingira ya kazi

Doctor patient ratio mpaka sasa kwa nchi yetu bado hairidhishi kabisa

Kuhusu Mama kumpasua mwanaye ni Against code of ethics za kitabibu na sio kila daktari anaweza ku intervene IO
Hii habari imekaa kikuda
Shida ya kua kila mtu anataka kuwa first reporter
Maana haileti maana kusema kua hospital ya rufaa mgonjwa amsubiri daktar mmoja siku mbili, eti alikua anafanya operation ya mama
Kwanza ob/Gyn kivyake na surgical department ipo kivyake
There is something missing
I second you probably pt was on non surgical intervention probably for stabilization
 
Kwanini kusiwez na madtari wa kulipwa posho
.day workers doct. yupo mtaan ikitokea dokta muajiriw hayupo aitwe yeye afanye kazi alipwe
Kufka hospital kwa wakat na ukakosa huduma kwa wakat na kupelekea mauti au madhara mengine inaumiza sana

R.i.p, go too soon
 
Wakuu kifo cha huyo mwanafunzi kimeniuma sana japo hata simfahamu sababu hilo tatizo limeshanikuta.

kilichonifanya niumie zaidi ni maumivu aliyoyapata sababu nayajua nilishayapitia.

Baada ya operation kulazwa siku tano na kuruhusiwa nikasoma discharge form imeandikwa......
A patient suffered from "intestinal obstruction secondary to sigmoid volvulus'' He is doing better, passing slool and He is discharged.

Yaani tatizo langu ilikuwa ni zaidi ya intestinal obstruction(utumbo kujikunja) iyo secondary to sigmoid volvulus (yaani baada ya kujikunja na kuziba, tatizo lika develope utumbo ukavimba mvimbo mkubwa sana)

Madaktari walishangaa wanashangaa imekuwaje nikaweza kuishi na hilo tatizo mpaka lika develope kiasi hicho kumbe bana kilichokuwa kinanisaidia kila siku alfajiri nilikuwa nakimbia cross-country ndo chakula kitapita kwa tabu kwenye iyo brokadge, ndo maana ilikuwa kukata gogo ni mpaka nitoke running.

Siku ya kuugua kila kitu nachokula kina rudi chochote hata maji natapika, nasikia mpwito nikienda toi sikati gogo narudi ndani tumbo linauma kinyama siwezi kutembea wima nimenyooka, urefu wangu ni futi 6 na nchi 3 takini nilikuwa natembea kimo cha futi 3 kupunguza maumivu.


kufupisha nilienda hospitali usiku saa nane, kelele nilizokuwa napiga yaani kila mtu ile hospitali alijua hapo tatizo bado halijajulikana nimepigwa drip tu nasikia maumivu kinyama.

pakakucha maumivu ni makali nikaambia nesi maumivu nayosikia ni makali sana, hee nesi anasema dirisha la dawa bado kufunguliwa nisubili wafungue (hapo nilikuwa na bima ya NHIF) ikabidi dawa ya maumivu ikanunuliwe mtaani ikaletwa nesi akanichoma sindano.

ile sindano sikuisikia wakati anachoma, nikamiuliza tayari ushachoma akasema eeeh maajabu ile sindano ya kutuliza maumivu haikusaidia chochote maumivu ndo yakaongezeka mpaka saa tatu ndo kupelekwa utra sound ndo tatizo kujulikama hapo napiga mwano kinyama.

kule utra sound aliyekuwa ananifanyia examination kwa sababu nimelala sioni kwenye monitor nikamuuliza shida ni nini? akawa anajidai hii mashine mbovu yaani hata haionyeshi vizuri, nikamuambia nilisoma psychology chuo najua unachokifanya wewe nambie tu shida nini mimi naweza ku handle taarifa yoyote lakini hakunambia.

nikarudi wodini nikaambiwa natakiwa nifanyiwe emergency operation, nesi akaja kuniandaa nisaini operation ifanyike, sikuwa na weza ku saini alisaini girlfriend wangu, huyu ndo alienipeleka hospitali baada ya kuona hali yangu sio nzuri kulala geto mwenyewe nilimpigia simu jana yake nilikuwa nae gheto.

nikaandaliwa ule mpira wa mkojo unapitishwa kwenye mashine na nesi mrembo(ila hamfikii shemeji yenu) nmejikaza muda huo sipigi kelele naambiwa pole utapona, kamaliza anasukuma kitanda kwenda theater kuna ka umbali nikashindwa kuvumilia maumivu nilipiga kelele nazani hakuna mtu kwenye ile hospitali aliyewahi kupiga kelele kubwa vile yaani wanaojifungua walikiwa wananiulizia hizo kelele zinatoka wapi?

kule theater nikawekwa kwenye kitanda, nikaunganishwa nyaya nyaya zile, akapachika sindano kwenye kile kidude cha drip nilikiwa nacho mkononi nikalazwa chali pozi nimetanua mikono.

nikamuambia yule jamaa hilo pozi naumia nigeuke akaniruhusu, hapo bado wawengine wanavaa Sergio anasubiriwa, maama ilikuwa emergency halafu ilikuwa jumatano sio siku ya operation maama ile hospitali ni ya wilaya na tu, Operations zote huwa wana zi schedule juma nne na alhamis.

Eeh wana chelewa kuja maumivu makali hapo kile ki sindano sijui cha nini kipo kwenye mkono, yule mwamba alokiweka na yeye yupo. kichwa nikafikiria hiki ki sindano ni cha kunizima nikapata wazo nikipushi nizime maana maumivu ni makali sana, yaani muda huo nilikuwa natamani hata nife,

ite natala kupush dawa yule mwamba aliniona alifoka UNATAKA KUFANYA NINI UTAKUFA halafu akaniweka lile pozi chali bila kujali maumivu ya lile pozi sikujua kilichoendelea tena baada ya masaa mawili na nusu ndo natoka theater.

yale maumivu ya usiku niliongea na maza girlfriend akawa anampa updates, kipindi naenda theater maza akafunga safari kutoka mkoa mwingine maama mimi niko kikazi mkoa mwingine. natoka theater akapewa updates.

nimekuja kushtuka usiku bi mkubwa kashafika, wafanya kazi wenzangu ofisini wapo hawaamini maana jana yake siku niliyoanza kuumwa nilikwepo kazini.

Keshoyake Dr anapita swali ya kwanza kuulizwa "umejampa" nikamwambia ndio akanamia safi hiyo ni hatua nzuri ndo kujua kumbe kujampa ni suala la msingi sana, akanambia unaweza kutembea nikamuambia ndio bas nika natembea mule room napita kwenye korido ila natembea kizombi kuna mtu pembeni yuko standby kunidaka.

Dr alikuja kutoa lile bandage hee kuona mshono mrefu na hivi mimi ni mrefu yaani tumbo lote vertical umeshonwa nyuzi 27, nikawa naogopa kutembea nahisi mshono utafumoka utumbo umwagike kumbe ni kutu ambacho hakiwezekani.

kuruhusiwa nikaenda geto kuuguza mshono hapo, hapo huduma zote kupikiwa chakula, kupelekwa haja ndogo na kubwa, kusafishwa, kubadilishwa nguo kila kitu anafanya yule girlfriend wangu, maza hana kazi alivoona naendelea vizuri na huduma zote napata akanambia hata akiondoka nikamuambia poa akasepa kuendelea na majukumu yake.

Kabla hajaondoka maza alinambia huyu mwanamke wako usimuache nikamuuliza kwa nini hata hakunambia chochote, bas bana niliuguzwa huku nikiwa comfortable nakiri sidhani kama ningekuwa comfortable kama ningeuguzwa na mtu yoyoye mwingine, vuta picha unataka kwenda kukata gogo upekekwe ushikiliwe kwenye kukaa huko chooni umalize umwagiwe maji kujisafisha ufutwe majimaji uvalishwe urudishwe ndani.

Hizo kazi ni mara 100 azifanye mwanamke wako utakiwa comfortable kuliko azifanye mama yako. huwa nawashangaa kataa ndoa hawafikirii siku wakiugua,

Girlfriend wangu kabla ya mimi kuugua nilikuwa nimesha mpaga assignment kibao(bila yeye kujua) za kuwa mke alikuwaga amesha pass hizo assignment sema bado nilikuwa sijatangaza kumuoa. akanipa bonus ambayo sikumuambia maana aliachq kazi alikokuwa anafanya ili aniuguze saivi ni mke wangu halali na tuna watoto.

Kuhusu kutuliza mshono, nilikuwaga sielewi maana yake nilikuwa najua ni msemo tu wa kumwambia mtu atulie, nikajua baada ya kuupata mshono yaani inatakiwa uutulize tena usiwe na haraka utembee kizombi hashwaaa maana ukiutikisa mshono ni hatari,

kuna siku naenda hospita waangalie maendeleo wa mshono, chombo nimepanda dereva akapita kwenye vile vituta vidogovidogo kwa speed grrrriiiiii ebanae ndo nikaelewa maana ya kutuliza mshono.

Samahani kwa hili bandiko refu nimejikuta tu naandika nimemuhurumia sana huyo kijana maumivu aloyapata sababu I felt the same pain.
Pole Sana Mkuu Kwa uliyopitia japo usimuliaji wako umenichekesha,hapo kwenye kutuliza mshono nilifanyiwa OP nilivyoruhusiwa nikaja kuchukuliwa na Prado aisee gari ikipita kwenye vile vituta hayo maumivu Yake mpka nikawauliza hivi mna uhakika hii ni gari au tumepanda toroli jamani!!
Tumeingia rafu road ni karibu na nyumbani nikawaambia wanishushe nitembee Kwa miguu!!!
 
Kama hujawahi kushuhudia uzembe unaofanyika mahospitalini huwezi kuelewa hii thread!!
Lakini mkuu hapo kwenye laki nane nadhani hamkumtafuta mama yake kwanza mkafanya maamuzi ya kumhamisha!!
Maana hata muuza genge Kwa inshu hiyo angekopa hata kausha ili mtoto atibiwe!!!
Rest in peace kijana mdogo
Nb; uzembe mahospitalini upo tuchukue tahadhari!!!
 
Hospital ya mkoa sio kituo cha afya au hospital ya wilaya
Wapo department wise, hivyo general surgery inajitegemea haingiliani na obs/Gyn, correct me if I'm wrong
Labda kuna ishu ingine lkn hiyo ya kua daktar alikua anafanya operation ya mama sidhani
Uko sahihi,ila huduma zetu zaafya ziko poor,tutafute hela na network pale muhimbili au uende Agha Khan,hizi za mkoa sijui wilaya ni kudanganyana tu,hata uchunguzi ukifanyika trust me doctor itaonekana hana kosa,maana unaweza kuta kulikuwa na watu wenye emergency case wengi kuliko anavyoweza kuamini,sitaki kuamini kuwa doctor alikuwa busy anachat au anakunywa chai
 
Mwanamke akijifungua mimba ya kwanza mara nyingi wote mnakuwa hamjui jinsi ya kuhudumia ndo maana wengi wanaenda kuhudumiwa,

mimba ya pili wife alivojifungua sikuruhusu aende, alinifundisha vile alikuwa anahudumiwa kwenye mimba ya kwanza nikawa namuhudumia mimi kwa kufuata maelekezo anayonipa ndo kujua
Aisee Mungu azidi kuwatunza
 
Back
Top Bottom