Kilimo
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 777
- 194
Ndugu wanaJF "MKASI NA PAMBA ILIYOKUWA IKIFUTIWA DAMU" VYAKUTWA TUMBONI BAADA YA OPERESHENI YA PILI
Kwa mujibu wa mfanyakazi mwenzangu, kuna binti mmoja alijifungua/kuzaa kwa njia ya oparesheni kama wiki tatu hivi zimepita pale hospitali ya Tumbi iliyopo kibaha mkoani Pwani, baada ya kutoka hospitalini kama wiki moja hivi alianza kuhisi maumivu makali tumboni mwake na baadae kidonda chake kikaanza kutoa usaha iliyopelekea nduguze kumrudisha tena hospitalini, Tumbi, akafanyiwa vipimo ikaonekana kuna vitu ndani ya tumbo hivyo basi inabidi mshono ufumuliwe ili mkasi na pamba vitolewe kwa uhai wa yule binti.
Operesheni ilifanikiwa, ingawa siyo kwa yule dokta wa awali kwa mujibu wamleta habari, maana mgonjwa alizinduka lakini baada ya masaa kadhaa hali ya mgonjwa ikawa mbaya na kupelekea kufanya jitihada za kumhamishia hospitali ya Lugalo ambapo alikubaliwa vile tu baba wa huyo binti anafanyakazi pale, ni mwanajeshi, pia bado hali yake inazidi kuwa mbaya hadi leo ndugu zake wamezuiliwa kumjulia hali.
Kwa mujibu wa mleta habari, kulikuwa na madaktari wanaojifunza, interns, mbao walikuwa kwenye jopo la waliomfanyia operesheni.
Hitimisho.
Kwanini hizi kesi au mikasa ya mahospitalini iwahusuyo madokta na wasaidizi wao haishi? au wanabambikiziana?
kweli Tanzania yetu bado haijakamilika!
Mida hii ya saa22.20 napigiwa simu kuelezwa kuwa yule mgonjwa hatimae KAFARIKI, RIP, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake Lihimidiwe maana na itakumbukwa kwa kila chenye uhai lazima kionje umauti!