Uzembe wa hospitali ya tumbi kibaha, mgonjwa yu mahututi sasa pale hospitali ya lugalo jeshini

Kilimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
777
Reaction score
194
Ndugu wanaJF "MKASI NA PAMBA ILIYOKUWA IKIFUTIWA DAMU" VYAKUTWA TUMBONI BAADA YA OPERESHENI YA PILI

Kwa mujibu wa mfanyakazi mwenzangu, kuna binti mmoja alijifungua/kuzaa kwa njia ya oparesheni kama wiki tatu hivi zimepita pale hospitali ya Tumbi iliyopo kibaha mkoani Pwani, baada ya kutoka hospitalini kama wiki moja hivi alianza kuhisi maumivu makali tumboni mwake na baadae kidonda chake kikaanza kutoa usaha iliyopelekea nduguze kumrudisha tena hospitalini, Tumbi, akafanyiwa vipimo ikaonekana kuna vitu ndani ya tumbo hivyo basi inabidi mshono ufumuliwe ili mkasi na pamba vitolewe kwa uhai wa yule binti.
Operesheni ilifanikiwa, ingawa siyo kwa yule dokta wa awali kwa mujibu wamleta habari, maana mgonjwa alizinduka lakini baada ya masaa kadhaa hali ya mgonjwa ikawa mbaya na kupelekea kufanya jitihada za kumhamishia hospitali ya Lugalo ambapo alikubaliwa vile tu baba wa huyo binti anafanyakazi pale, ni mwanajeshi, pia bado hali yake inazidi kuwa mbaya hadi leo ndugu zake wamezuiliwa kumjulia hali.
Kwa mujibu wa mleta habari, kulikuwa na madaktari wanaojifunza, interns, mbao walikuwa kwenye jopo la waliomfanyia operesheni.

Hitimisho.
Kwanini hizi kesi au mikasa ya mahospitalini iwahusuyo madokta na wasaidizi wao haishi? au wanabambikiziana?
kweli Tanzania yetu bado haijakamilika!

Mida hii ya saa22.20 napigiwa simu kuelezwa kuwa yule mgonjwa hatimae KAFARIKI, RIP, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake Lihimidiwe maana na itakumbukwa kwa kila chenye uhai lazima kionje umauti!
 
stori yako imenitoa chozi, inahuzunisha sana
 
Hii Nchi Hospital ni maeneo ambayo yanasababisha vifo kuliko kwa waganga wa kienyeji

Jirani yangu alifanyiwa upasuaji wa uzazi mwezi wa sita mwanzoni pale Tumbi, baada ya wiki 2 akasikia maumivu makali na kidonda hakiponi, aliporudishwa wakasema kuna tatizo wakampasua tena, after wiki 2 akaanza kutoa harufu kali sana mdomoni anapoongea na kidonga hakiponi, Tumbi wakagoma kutoa transfer ya kumpeleka muhimbili wakamfanyia upasuaji mwingine wa tatu..Wiki iliyopita amefariki...
Sijui ni nini kinatakiwa kifanyike kwani serekali yetu haijali lolote zaidi ya kufanya siasa tu. Ukizingatia Hospital ya Tumbi imepandishwa hadhi na kuwa hospital ya Rufaa sijui tunaelekea wapi?
R.I.P Mama Kidevu
 
Dah jamani poleni saana
Kuna tatizo kuwa kwenye Sector nzima ya afya Tanzania.......kitu ambacho wanasiasa hawataki kabisa kukisikia.....kumbukeni dr. Ulimbka alisema vifo vinavyotokea hospitalini kwa kukosa vifaa..uzembe..ni vingi ukilinganisha vilivyotokea kipindi kile walipogoma....kumbukeni ni ngumu saana jamii kushtuka kwani vinagusa watu wachache na vingi vinafunikwa

Kuna tatizo kubwa saana na taaluma za hawa madaktari......kuna vyuo vinazalisha madaktari lakini....havina sifa hata kidogo na hivyo vyuo vinajulikana kabisa...ila wanasiasa wamesinzia kwakuwa wao na jamaa zao kama sio India ni SA kama sio ni Nairobi wanapata matibabu....
 
duuuu avata na hii taarifa yako inaonyesha wewe ni muongo
 
Tatizo tulilonalo sisi wabongo ni kuwa hatujui maana ya hasa ya neno KUWAJIBIKA.
 
Hii Nchi Hospital ni maeneo ambayo yanasababisha vifo kuliko kwa waganga wa kienyeji

Jirani yangu alifanyiwa upasuaji wa uzazi mwezi wa sita mwanzoni pale Tumbi, baada ya wiki 2 akasikia maumivu makali na kidonda hakiponi, aliporudishwa wakasema kuna tatizo wakampasua tena, after wiki 2 akaanza kutoa harufu kali sana mdomoni anapoongea na kidonga hakiponi, Tumbi wakagoma kutoa transfer ya kumpeleka muhimbili wakamfanyia upasuaji mwingine wa tatu..Wiki iliyopita amefariki...
Sijui ni nini kinatakiwa kifanyike kwani serekali yetu haijali lolote zaidi ya kufanya siasa tu. Ukizingatia Hospital ya Tumbi imepandishwa hadhi na kuwa hospital ya Rufaa sijui tunaelekea wapi?
R.I.P Mama Kidevu

kweli hii inatisha sana, sasa kama na hilo lilitokea hapo maanayake hapo kuna tatizo, yawezekana kuna upungufu wa madokta wenye sifa, maspesholisti, au tatizo jingine sasa uchunguzi wa tume huru ndiyo utatoa majibu sahihi kwa pale tumbi.
 
duuuu avata na hii taarifa yako inaonyesha wewe ni muongo

kwanini mwongo? Umefuatilia umeona cyo kweli? Tupe ukweli wako unaojua juu ya hayo yasemwayo!
 
Dah jamani poleni saana
Kuna tatizo kuwa kwenye Sector nzima ya afya Tanzania.......kitu ambacho wanasiasa hawataki kabisa kukisikia.....kumbukeni dr. Ulimbka alisema vifo vinavyotokea hospitalini kwa kukosa vifaa..uzembe..ni vingi ukilinganisha vilivyotokea kipindi kile walipogoma....kumbukeni ni ngumu saana jamii kushtuka kwani vinagusa watu wachache na vingi vinafunikwa

Kuna tatizo kubwa saana na taaluma za hawa madaktari......kuna vyuo vinazalisha madaktari lakini....havina sifa hata kidogo na hivyo vyuo vinajulikana kabisa...ila wanasiasa wamesinzia kwakuwa wao na jamaa zao kama sio India ni SA kama sio ni Nairobi wanapata matibabu....

ni kweli hospitali nyingi zina upungufu wa vifaa na ule mgomo wa madaktari moja ya madai yao yalikuwa ukosefu wa vifaa ingawa hata kwa maslahi wanapata kiduchu, maslahi ya madaktari ambao wameshika uhai wa binadamu pamoja na vifaa vya kitabibu , hv vyote ni lazima viboreshwe na serikali inayothamini wananchi wake, kwa rasilimali zetu tu bila msaada toka nje twaweza kuboresha mifumo yetu ikiwa pamoja na afya, yote haya yatawezekana tu tukiwa na serikali sikivu yenye maadili mema na inayomwogopa Mungu.
 
Mbona tunakoma wavuja jasho manake hatuna uwezo hata wa kumpeleka mgonjwa agha khan sembuse India. Tuna tatizo kubwa sekta hii na hasa huu utaratibu wa kulindana ndio unatuangusha zaidi. Hebu ona ktk hayo matukio yote 2 nani kawajibishwa. Lkn angefanyiwa binadamu ungeuona mziki wake afadhali limetokea kwa mtu.
 
ni kweli hospitali nyingi zina upungufu wa vifaa na ule mgomo wa madaktari moja ya madai yao yalikuwa ukosefu wa vifaa ingawa hata kwa maslahi wanapata kiduchu, maslahi ya madaktari ambao wameshika uhai wa binadamu pamoja na vifaa vya kitabibu , hv vyote ni lazima viboreshwe na serikali inayothamini wananchi wake, kwa rasilimali zetu tu bila msaada toka nje twaweza kuboresha mifumo yetu ikiwa pamoja na afya, yote haya yatawezekana tu tukiwa na serikali sikivu yenye maadili mema na inayomwogopa Mungu.

Inauma pale ambambo mtu alitakiwa asife lakini kutokana na uzembe..na kutojali kwa serekali watu wasio na hatia kila kukicha wanapoteza maisha...............Naamini ingekuwa wanasiasa na wao.....pamoja na familia zao...wanatibiwa hospitali za wilaya...mikoa..na rufaa...huu uzembe/na kutokujali ungeshakuwa historia.......hawa jamaa hawana uchungu hata kidogo..........kuna tatizo kubwa saana kwenye mfumo mzima wa kufundisha madaktari kwa ujumla ktk kada nzima ya afya......baada ya vyuo binafsi kuanza kufundisha madaktari.....na kumaliza kumekuwa kukiripotiwa matukio ya kusikitisha saana......siku hizi unaenda unaumwa kichwa unaandikiwa dawa za tumbo.....inatia huruma saana....na niwakati wanasiasa waambiwe ukweli sasa
 
Ndugu wanaJF "MKASI NA PAMBA ILIYOKUWA IKIFUTIWA DAMU" VYAKUTWA TUMBONI BAADA YA OPERESHENI YA PILI

Kwa mujibu wa mfanyakazi mwenzangu, kuna binti mmoja alijifungua/kuzaa kwa njia ya oparesheni kama wiki tatu hivi zimepita pale hospitali ya Tumbi iliyopo kibaha mkoani Pwani, baada ya kutoka hospitalini kama wiki moja hivi alianza kuhisi maumivu makali tumboni mwake na baadae kidonda chake kikaanza kutoa usaha iliyopelekea nduguze kumrudisha tena hospitalini, Tumbi, akafanyiwa vipimo ikaonekana kuna vitu ndani ya tumbo hivyo basi inabidi mshono ufumuliwe ili mkasi na pamba vitolewe kwa uhai wa yule binti.
Operesheni ilifanikiwa, ingawa siyo kwa yule dokta wa awali kwa mujibu wamleta habari, maana mgonjwa alizinduka lakini baada ya masaa kadhaa hali ya mgonjwa ikawa mbaya na kupelekea kufanya jitihada za kumhamishia hospitali ya Lugalo ambapo alikubaliwa vile tu baba wa huyo binti anafanyakazi pale, ni mwanajeshi, pia bado hali yake inazidi kuwa mbaya hadi leo ndugu zake wamezuiliwa kumjulia hali.
Kwa mujibu wa mleta habari, kulikuwa na madaktari wanaojifunza, interns, mbao walikuwa kwenye jopo la waliomfanyia operesheni.

Hitimisho.
Kwanini hizi kesi au mikasa ya mahospitalini iwahusuyo madokta na wasaidizi wao haishi? au wanabambikiziana?
kweli Tanzania yetu bado haijakamilika!

Mida hii ya saa22.20 napigiwa simu kuelezwa kuwa yule mgonjwa hatimae KAFARIKI, RIP, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake Lihimidiwe maana na itakumbukwa kwa kila chenye uhai lazima kionje umauti!

RIP ndugu yetu,But Habari za kitaaluma kama hizi za kusimulia kiswahili hivyo ndugu yangu,mgonjwa alifanyiwa operation,we umekimbilia tu kwenye kusahau mikasi na pamba!!Wajuaje kwamba pengine baada ya operation ya kwanza ya mgonjwa,kidonda hakikukutunzwa vizuri akadevelop sepsis ambayo ikapelekea kufanyiwa resuturing ,though sepsis ikaendelea kutokuwa managed well na kusababisha kifo cha mgonjwa?punguzeni ukanjanja kwenye taaluma,ndo maana huwezi ukakuta kwenye suala kama hili hata ikiundwa tume lazima majority wawe ni wale wenye taaluma hiyo kuepusha uswahili wenu mara hii ikawa vile,alikutwa na mbao tumboni,ohho chura alikutwa kwenye koo!!!
 
sawa mkuu umeongea ukweli juu ya taaluma ila nami pamoja na wachangiaji wengine hatujamnyooshea kidole daktari mojakwamoja, kuna vitu vingi vyaweza kuwa vimechangia hapo lakini mkasi pamoja na pamba zenye damu vilikutwa tumboni kwa mgonjwa alipofanyiwa operesheni ya pili.
 
Kwakweli hiyo hospital ya tumbi imezidi......mimi mwenyewe nimenusurika kufa pale!!nilifanyiwa opareshen ya uzaz,wakaniambia niende kutoa nyuz after 7days nilivyoenda baada ya kutoa nyuz kidonda kikawa bado hakijafunga kbsa,wakaniambia inabid wanishone tena,sasa hilo zoez la kushonwa tena lilichukua km wiki mbili baada ya kuto zile nyuz za kwanza......kila cku walikuwa wananizungusha kila cku nikienda naambiwa docta wa kunishona hayupo,wananipangia tarhe nyingine!!sasa baada ya kushonwa tena nimekaa wiki km mbili hv tumbo likaanza kuniuma mno,natapka na kuishiwa nguvu......nikirud tumbi hamna wanachoniambia!!!ndo nikaomba transfer ya kwenda muhimbili(tena hyo transfer nayo niliipata kwa shida),muhimbili wakaniambia nna tatizo tumbon inabid nifanyiwe tena oparation tena.....;kwakwelihali yangu ilikuwa mbaya sana ht kutembea nilikuwa cwez!!ila baada ya kufanyiwa oparation pale muhimbil nashukuru mungu nilipona!!

kesi nyingi sana km hiz zinatokea pale tumbi,......madaktar inabid wawe makin waache uzembe!!
 
Back
Top Bottom