demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Wilayani Kyela, Katika kata ya Serengeti siku ya jumamosi 27-02-2021 ilipata kuanguka nguzo mojawapo ya umeme wa Tanesco Hata kukapelekea kukosekana kwa umeme katika katika kata hiyo. Ikumbukwe leo ni Ijumaa ya tarehe 05-03-2021.
Wana-Serengeti wakafanya jitihada ya kuwasiliana na mamlaka za umeme (Tanesco Kyela - 0787028355) ili waweze kufanya marekebishi ya nguzo hiyo kwa sababu ilikuwa imedondoka katika maeneo ambapo watoto wanapenda kucheza cheza na pia kuweza kurejesha huduma za umeme haraka kwa wakaazi wa eneo hilo.
Cha kushangaza tangu wapewe taarifa ya kudondoka kwa nguzo hiyo wameshindwa kuchukua hatua stahiki na haraka zaidi. Ukijaribu kuwasiliana nao wanatoa majibu ya ajabu ajabu wa wananchi. Tangu jumapili ya wiki iliyopita mpaka leo hii ni siku 6 zimepita hawajafika katika eneo ili kutimiza wajibu wao. Wananchi wamekuwa wakidhani labda idara ya tanesco ya umeme haina pesa ili kuweza kulipa mafundi waje kutimiza wajibu hata wakajaribu kuona uwezekano wa kuchangisha mapema ili zoezi lianze.
Jioni ya leo mmoja wa mwanafunzi wa shule ya msingi ajulikanaye kawa jina la Albert Mwakajila (6) amefariki kutokana na kuchezea nyaya ya umeme ambayo imedondoka na nguzo hiyo.
Wananchi wa kata ya Serengeti wanaomba msaada kutoka ofisi za Tanesco mkoani mbeya ili kufuatilia suala hili mapema iwezekanavyo ili kuondoa hatari ya umeme kwa watoto wa eneo hilo.
Kata ya Serengeti wilayani Kyela imekosa umeme tangu siku ya jumamosi usiku wa tarehe 27-02-2021
Nawasilisha.
UPDATES:
Baadaya ya kubandikwa kwa bandiko hili. Leo mchana tanesco wamefika enelo la tukio na kuanza kuchimba mashimo ya kusimamisha nguzo 2 zilizo anguka wiki iliyopita.