Uzembe wa TANESCO, Nguzo iliyo anguka yaua Mwanafunzi Kyela

Uzembe wa TANESCO, Nguzo iliyo anguka yaua Mwanafunzi Kyela

We jamaa huwa unajibu kama roboti, yaani unaudhi sana, unakera mna jinsi unavyojibu, laiti ningekujua niknhekufuata ulipo nikutandike vinao, jibu kama binadamu mwenye utashi na ubongo kichwani kwake, damn it!
Tatizo ni nini hasa?
Huyu bwana amefanya follow-up na kuleta mrejesho kuwa hakuna ajali yoyote iliyotokea zaidi ya nguzo kuinama, na aliyeleta tuhuma athibitishe beyond reasonable doubt. Sasa weye povu linakutoka, why??
 
Wilayani Kyela, Katika kata ya Serengeti siku ya jumamosi 27-02-2021 ilipata kuanguka nguzo mojawapo ya umeme wa Tanesco Hata kukapelekea kukosekana kwa umeme katika katika kata hiyo. Ikumbukwe leo ni Ijumaa ya tarehe 05-03-2021.

Wana-Serengeti wakafanya jitihada ya kuwasiliana na mamlaka za umeme (Tanesco Kyela - 0787028355) ili waweze kufanya marekebishi ya nguzo hiyo kwa sababu ilikuwa imedondoka katika maeneo ambapo watoto wanapenda kucheza cheza na pia kuweza kurejesha huduma za umeme haraka kwa wakaazi wa eneo hilo.

Cha kushangaza tangu wapewe taarifa ya kudondoka kwa nguzo hiyo wameshindwa kuchukua hatua stahiki na haraka zaidi. Ukijaribu kuwasiliana nao wanatoa majibu ya ajabu ajabu wa wananchi. Tangu jumapili ya wiki iliyopita mpaka leo hii ni siku 6 zimepita hawajafika katika eneo ili kutimiza wajibu wao. Wananchi wamekuwa wakidhani labda idara ya tanesco ya umeme haina pesa ili kuweza kulipa mafundi waje kutimiza wajibu hata wakajaribu kuona uwezekano wa kuchangisha mapema ili zoezi lianze.

Jioni ya leo mmoja wa mwanafunzi wa shule ya msingi ajulikanaye kawa jina la Albert Mwakajila (6) amefariki kutokana na kuchezea nyaya ya umeme ambayo imedondoka na nguzo hiyo.

Wananchi wa kata ya Serengeti wanaomba msaada kutoka ofisi za Tanesco mkoani mbeya ili kufuatilia suala hili mapema iwezekanavyo ili kuondoa hatari ya umeme kwa watoto wa eneo hilo.

Kata ya Serengeti wilayani Kyela imekosa umeme tangu siku ya jumamosi usiku wa tarehe 27-02-2021
Nawasilisha.
Umeshindwa kabisa hata kuweka picha ya nguzo iliyodondoka?
Tupia hapa jukwaani hata picha ya msiba.
 
Umeshindwa kabisa hata kuweka picha ya nguzo iliyodondoka?
Tupia hapa jukwaani hata picha ya msiba.
Nimekuelewa ulivyohitaji picha ya eneo.

Ila umenishangaza ulipo hitaji hadi picha za msibani. Mungu akuongezee hekima kijana.
 
Ndugu mpendwa mteja wetu

Tumefatilia kwa kina mpaka kwa uongozi wa eneo husika hakuna nguzo iliyoanguka bali ziliinamana na kazi ya kuzibadilisha ilishindikana kutokana na uwepo wa nyuki wengi kwenye nguzo hizo.Usiku wa kuamkia leo tumefanikiwa kuondoa nyuki na sasa zitabadilishwa.Aidha hakuna kifo chochote kilichotowe taarifa au kutokea eneo husika hivyo kama una taarifa ya ziada weka hapa na namba yako tukusikilize.

Imagine TANESCO wanakwambia walishindwa kufanya kazi kwa sababu ya Nyuki, yaani TANESCO wanaogopa nyuki kuliko umeme.

Yaani nisinge weka hili bandiko hapa basi bila shaka wananchi wa kata ya serengeti wangekaa bila umeme kwa zaidi ya mwezi & pengine watoto zaidi wangekufa kutokana na nyaya za umeme zilizokuwa wazi njiani.
 
Tanesco mnathibitisha udhaifu wenu hadharani.

Ina maana baada ya malalamiko ya kuwa nguzo imeua ndiyo mkaja na majibu ya kukanusha?

Kama malalamiko hayo yasingekuwepo maana yake hakuna kazi ingefanyika.

Hao nyuki waliwashinda akili hapo kabla. Ila leo dawa ndiyo imepatikana. Rungu Spray iliwashinda kununua?

Pathetic!...
Yaani Tanesco hawawezi kuua Nyuki eti.
 
Tatizo ni nini hasa?
Huyu bwana amefanya follow-up na kuleta mrejesho kuwa hakuna ajali yoyote iliyotokea zaidi ya nguzo kuinama, na aliyeleta tuhuma athibitishe beyond reasonable doubt. Sasa weye povu linakutoka, why??
Ni kipi hasa hujaelewa katika nilichoandika? Hujui kusoma au una shida ya kuelewa? Huyu jamaa huwa kuna nyuzi nyingi sana humu huwa anajibu kuhusu Tanesco, nenda kazisome walau chache tu, then uone jinsi anavyojibu, ni kama roboti.
 
Tunashukuru sana

Taarifa imejibiwa aliyejibiwa hakutoa ushahidi au kukanusha je robot gani angweza kufatilia na kujibu

Wakati mwingine tushukuru hata Shirika kuona umuhimu wa kuwajibu taarifa zenu humu
 
Tumepokea taarifa kwa ufatiliaji na hatua zaidi.
Mnazingua sana tena sana,,swala la nguzo kuanguka ni la haraka mno maana madhara yake ni makubwa sn,,kweli hamkujua yanayoweza kutokea,,maana hii ni sawa na jengo linaloungua kwa watu wa fire,,,ukweli mnakera
 
Tunashukuru sana

Taarifa imejibiwa aliyejibiwa hakutoa ushahidi au kukanusha je robot gani angweza kufatilia na kujibu

Wakati mwingine tushukuru hata Shirika kuona umuhimu wa kuwajibu taarifa zenu humu
Hivi sasa unajibu kama binadamu, hivi ndivyo unatakiwa uwe unajibu na kuzungumza na watu, sio kutoa majibu mafupi ya mkato na yasiyo na mantiki kama preprogrammed computer isiyo na utashi.
Cha zaidi, kujibu hoja zinazowahusu ni wajibu na si favor kuwa mshukuriwe, kuna kitengo cha mawasiliano na mnalipwa. Na usinijibu tena, yaishe.
 
Tanesco wana structure mbovu kiutendaji na ndio maana emmergence nyingi wanashindwa kizitatua mapema.

On other side workers wao wana schedule nzito mno, inawezekana idara ya construction ikawa na kazi kama 23 kwa siku moja, hata kitengo cha emmergence kinaweza kuhusishw a kwenye kazi za magroup mengine ili kufidia gap la idadi ya kazi.

I see nothing done after this
Kama usemacho ni kweli, basi wanahitaji kujirekebisha fasta. Watu wa emergency ni sawa na zimamoto huwezi kuwapa kazi nyingine kwa sababu yoyote ile.
 
Tunashukuru sana

Taarifa imejibiwa aliyejibiwa hakutoa ushahidi au kukanusha je robot gani angweza kufatilia na kujibu

Wakati mwingine tushukuru hata Shirika kuona umuhimu wa kuwajibu taarifa zenu humu

Tuwashukuru kwa kutujibu taarifa zetu? Mkuu unatudharau.. Kutujibu ni lazima na sio ombi, mnalipwa mshahara kwa kazi hiyo.
Na umeme hamtupi bure tunanunua kwa gharama kubwa iliyopitiliza.
 
Ndugu mteja,
Soma hapo juu tumetoa maelezo ya kina hakuna nguzo ilioanguka wala kusababisha kifo

Tunashukuru sana

Taarifa imejibiwa aliyejibiwa hakutoa ushahidi au kukanusha je robot gani angweza kufatilia na kujibu

Wakati mwingine tushukuru hata Shirika kuona umuhimu wa kuwajibu taarifa zenu humu
Aisee wewe ni afisa habari na huduma kwa wateja TANESCO??

Tumia akili kidogo nana busara na hekima, hata kama hujapata mafunzo stahiki, wacha kuliaibisha shirika, kwa kujibizana na wateja walio nyuma ya keyboard.

Tatizo limekwishatatuliwa hilo ndiyo la msingi, kujibizana humu ni kuliharibia shirika image. ACHA TAFADHALI!
Unaanza kuonekana rude, obnoxious, pompous & arrogant.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom