Uzembe wa TANESCO, Nguzo iliyo anguka yaua Mwanafunzi Kyela

Mpaka malori Yani, unakuta foreman anaenda kunywa chai ,hafu wafanyakazi wamekaa kwenye Lori wanamsubiria . Saa tatu au nne . Tena hili la kunywa supu mda wa kazi ni limeota mizizi Yani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Management wanajifanya hawalioni, kuna uwezekano huyu tunayejibizana naye humu ndiye mnywa supu ila anajishaua tu
 
Yaani whistle blower unataka atoe namba ya simu tena? Hivi wengine akili zenu zinafanyakazi kweli?? Amekueleza eneo cha kwanza kabisa ungecheki na ofisi zenu za huko Kyela ama ofisi ya serikali ya huko.
Brilliant!!!

Yeye amekaa kwenye keyboard anasubiri namba ya simu, hii ni ishara mojawapo kuwa hawana uwezo wa kazi, wanasubiri kuletewa badala ya kutafuta
 
UPDATES:

Baadaya ya kubandikwa kwa bandiko hili. Leo mchana tanesco wamefika enelo la tukio na kuanza kuchimba mashimo ya kusimamisha nguzo 2 zilizo anguka wiki iliyopita.
Halafu kuna kijamaa kijingakijinga kinajiita tanesco humu kinakanusha ati hakuna kitu kama hicho
 
Tatizo ni nini hasa?
Huyu bwana amefanya follow-up na kuleta mrejesho kuwa hakuna ajali yoyote iliyotokea zaidi ya nguzo kuinama, na aliyeleta tuhuma athibitishe beyond reasonable doubt. Sasa weye povu linakutoka, why??
Humuamini aliyeleta taarifa kwa kuwa labda hajaweka picha ila unaamini taarifa ya aliyefuatilia japo nae hajaweka picha. Ajabu sana!!

Unamtaka mtoa taarifa athibitishe tuhuma beyond reasonable doubt, jambo ambalo lingeweza kufanywa tu na TANESCO (wakati wa kukanusha taarifa /lalamiko) kwa kupiga picha ya hilo eneo ikionesha nyuki na hizo nguzo zilizolala. Kama ni nguzo zimelala na sio kuanguka kwa nini wao wasipige picha?
 
Mkuu ukiona Jamiforums hawajauondoa uzi hapa ujue wamefuatilia wamejiridhisha kuwa una ukweli, vinginevyo kama ingekuwa uzushi wangesha block jana ileile
 
Fanyeni tracking kwenye hiyo number iliyowasiliana nanyi siku hiyo na kwakuwa si jambo la kificho basi waliohusika na huo uzembe wawajibishwe maramoja kuliokoa shirika na lawama
Ukweli wanakera Sana,umeme ni nishati ya hatari ikiwa haiko kwenye usalama wa mtumiaji,lakini tanesco wamelisahau Hilo,wameuchukulia umeme Kama vile nishati ya kuni au mkaa!!!
 
Ni kweli kuna kifo kimetokea kwa ajili ya hiyo nguzo? Wenyewe wanasema hakuna kifo. Tuamini lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…