KERO Uzembe wa Wataalamu wa Afya na Mamlaka husika unavyoteketeza raia

KERO Uzembe wa Wataalamu wa Afya na Mamlaka husika unavyoteketeza raia

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nilitembelea hospitali kubwa za nchi hii 3, ni katika utaratibu wangu wa sadaka kama tunavoelekezwa katika biblia kwamba dini njema ni ile inayojali wajane, wagonjwa na maskini....

Sasa, sababu ya kuja hapa ni mambo ya hatari ambayo nimekua nikiyaona...aisee ugonjwa wa kansa unakuja kwa kasi sana.... watu wanaumwa huu ugonjwa kwa makundi na makundi.... .cha ajabu sioni juhudi za wataalamu wa afya kuingia field na kuja na majibu ya sababu ya kupanda kwa maradhi haya....

Ningeona watu wazima pekee, ningeelewa lakini kuna kundi kubwa la vijana tena wenye nguvu ambao wamekua diagnosed na huu ugonjwa....hii ilinipelekea kuweka malengo ya kufanya utafiti binafsi kwa sababu wanaotakiwa kufanya haya wako maofisini tu wanakula kiyoyozi.

Sababu nilizogundua ni kama zifuatavyo:

1. Ulaji mbovu wa haya mavyakula ya fast food, vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda, juice za mabox, energy drinks ( hizi zinaua sana vijana), vyakula vya kukaangwa sana na mafuta ya mbegu kama chipsi, kuku etc

2. utumiaji wa plastics kwenye vyakula vya moto, hili ni tatizo kubwa sana kuanzia kwa mama ntilie mpaka kwenye hotels, unakuta ugali wa mama ntilie wamoto anauweka kwenye nailoni ndani ya sufuria ili usipoe....hii ni sumu mbaya sana....yani unashangaa kijana mbeba mizigo kkoo anakansa unakua huelewi...kumbe anakula sumu ya nylon kutoka kwenye ugali wa mama ntilie au mihogo ya moto inawekwa kwenye vile vimfuko vilaini vya nylon...hii inatakiwa pigwa marufuku mara moja.

3. chapati nyingi zinachomwa kwa kutumia sponji/sponge ile material ya godoro.....hii ni sumu moja mbaya sana, ingia youtube angalia namna godoro linatengenezwa....ni mchanganyiko wa chemicals ndio huleta godoro unapoliexpose kwenye joto kali kutoka kwenye kikaangio cha chapati ile sumu inatoka kwenye sponge inahamia kwenye chapati then ukila unaimeza sumu hiyo.

4. utumiaji wa alluminium foil....hili ni janga kubwa sana, nyama ya foil ni tamu sana ila unakula sumu ndugu yangu, serikali ipige marufuku matumizi ya alluminium foil.

5. Kupendelea kula nyama za kuchoma/mishikaki, nyama ya kuchoma inasabisha kansa kama haitachomwa kwa kufuata njia salama....hii njia inayotumika nchini ni very risky..... unapochoma nyama kwa kuweka nyama kwenye zile nyavu alafu unaweka juu ya moto hua inadondosha lile jasho ambalo likidondokea kwenye moto hutoa umoshi mzito....ile sasa ndo kansa yenyewe.....

Ukiangalia wachoma nyama wengi wakongwe hufa kwa kansa mapafu....unashangaa mtu havuti sigara lakini anaambiwa ana kansa ya mapafu...chanzo chake ni hiyo.... ingine ni ile cabon inayobaki kwenye nyama ( nyama inakua imeungua hivi inaacha kama masizi hata kwenye nyavu inakua na masizi yalionasia ) ile ni mbaya sana.... ni kansa pure. Uchomaji nyama njia salama ni ule unakinga mafuta yale kwenye chombo ulichoweka maji alafu unafunikia kama unapalia wali....na kuweka moto mkali kuzunguka hiko chombo....usichome nyama kwa kuweka direct juu ya moto....

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yako common sana mitaani kwetu, hawa wadau wa afya wanaweza piga marufuku wakaokoa maisha ya watz pia kupunguza cost ya taifa kuuguza wananchi wake... badala ya kukaa ofisini watembee na kuelimisha wananchi....tunaangamia, kama hujawahi uguza mgonjwa wa kansa huwezi nielewa....

Mungu atusimamie.
 
Kansa ipi inaongoza kwa hao vijana kwa mujibu wa utafiti wako?
 
Ni muhimu serikali kuweka mkazo sana kwenye kutoa elimu ya kujikinga na kuzuia viashiria vyote ulivyovitaja. Hapo umezungumzia saratani pekee lakini ugonjwa wa kisukari ni kama mlipuko kwa sasa wagonjwa ni wengi tena wa rika zote. Mwisho, bado narudi kwa serikali kuweka mkazo wa elimu kwenye Televisheni na vipindi vya redio la sivyo tujiandae kwa bajeti kubwa ya afya ili kuhudumia maradhi hata.​
 
Ni muhimu serikali kuweka mkazo sana kwenye kutoa elimu ya kujikinga na kuzuia viashiria vyote ulivyovitaja. Hapo umezungumzia saratani pekee lakini ugonjwa wa kisukari ni kama mlipuko kwa sasa wagonjwa ni wengi tena wa rika zote. Mwisho, bado narudi kwa serikali kuweka mkazo wa elimu kwenye Televisheni na vipindi vya redio la sivyo tujiandae kwa bajeti kubwa ya afya ili kuhudumia maradhi hata.​
Mkazo wa elimu inamaanisha Serikali kupinga/ku-blackwash bidhaa ambazo zinachochea magonjwa (NCDs) hayo.

Je serikali iko tayari kupoteza kodi zitokanazo na Bidhaa hizo ili kunusuru Raia wake? Serikali iliyojaa mafisadi wenye kuangalia maslahi yao wenyewe.

Suluhisho lipo katika Raia wenyewe kujielimisha na kuacha matumizi ya Bidhaa zisizo rafiki kwa afya ya Binadamu, Tanzania hakuna Serikali ya kujali Raia wake. AFYA ni jukumu lako ndugu.

Nchini Tanzania kuna Ubinafsi wa kupindukia, Unafikiri wataalamu & mamlaka hazifahamu madhara ya Bidhaa hizo kwa Binadamu? Ni vile wanafikiri madhara hayatawafikia wao na wapendwa wao direct hivyo hakuna haja ya kudhibiti bidhaa hizo.

Pia ni lazima tufahamu kuwa Tupo katika Dunia ya Kibepari kwasasa, hivyo Faida/fedha ndo kitu kinachozingatiwa zaidi ya kitu kingine. Hivyo ni jukumu la kila Raia kuzingatia AFYA yake.

It's just the Beginning of the horror. It's the trailer.
 
Vipi kuhusu hizi sufuria za aluminium utafiti wako haukuangazia hapo

Niliacha kunitumia miaka ya nyuma baada ya kua ukichemsha maji yakipoa na kutulia pale juu unaona ka utando Fulani pia ukipikia mfano mboga yenye Nyanya halafu ikalala usiku kucha inatengeneza Kama reaction nikajua tu ni acid Ina react na aluminium

Kama aluminium foil sio salama basi zaidi ya asilimia 70 ya watanzania tayari wanaumwa au wameanza kuathirika maana hizi ndio sufuria zao
 
Back
Top Bottom