Uzi gani hutakaa uusome JamiiForums?

Uzi gani hutakaa uusome JamiiForums?

Uzi wowote uliiandikwa kwa kiingereza huwa sihangaiki nao, naona ni ukosefu wa uzalendo.

(Basi kuna watu watawaza eti sijui kiingereza).
 
Wasalaam Wakuu.

JF ni chuo kitaa. Unajifunza mengi mazuri na mabaya pia. Kama ambavyo chuo kuna kozi huwezi kuisoma, hata humu JF kuna nyuzi ambazo hutaki kuisoma kwa sababu moja ama nyingine.

Kichwa cha uzi kinabeba maana kubwa sana katika kumshawishi mtu kuusoma au kuupuzia. Na ndivyo ambavyo imekuwa kwangu.

Ukienda katika Jukwaa la JF Intelligence kuna uzi wenye kichwa 'Makosa 10 aliyofanya Mungu '

Pamoja na kuwa nauona kila siku sijawahi kuthubutu kuufungua. Binafsi, mimi ni muumi ni mkubwa sana kuwa Mungu yupo na ni muweza wa mambo yote kwa usahihi. Na hivyo, naamini Mungu hakosei katika maamuzi yake kwa utukufu alionao.

Ndiyo maana sikuona maana yeyote ya kuufatilia huo uzi. Pia, maandishi yana nguvu kubwa sana katika ushawishi. Kuusoma tu uzi ule kungeanza kujengeka picha katika ubongo wangu ni kwa namna gani Mungu alikosea na kufanya hivyo kungeanza kushusha kiwango cha imani yangu.

Hizo ndizo sababu zilizonifanya kuupuzia.

Je, wewe ni uzi upi ambao huwezi kuusoma na kwa sababu gani?
Siasa siasa na uchochezi
 
Kuna zile sjui zinaitwa CHOMBEZO... nazipitaga tuu
 
Uzi wowote wenye neno "tumpongeze Joni josefu"
 
Sijui mtu aliwaza nini kuanzisha, thread eti makosa aliyofanya MUNGU,niliusoma kwakuwa nilimuhurumia sana aliyeandika

Hata contents zenyewe hazina hata mashiko,ni vile tu watu kujitafutia laana.
 
Back
Top Bottom