Wezi wanabadisha mbinu za kuiba kulingana na mazingira hakuna uzoefu ndg yangu mimi waliniibia mchana jua linawaka. Walichofanya ni jambo rahisi tu,nilitoka sokoni mikono yote miwili nimebeba mzigo nikawa natembea simu iko kwenye mfuko wa shati,wezi walikuwa watatu, wakagawana wawili wakaenda uelekeo niliokuwa naenda moja akanifuata kwa nyuma,wale walioenda mbele wakarudi tukakutana mahali njia ni nyembamba yule wa nyuma akanikanyaga kwa nyuma ile nageuza shingo kuangalia kuna nini,wale tuliokuwa tunapishana moja kulia kwangu moja kushoto wakanichomoa simu wakati yule aliyekanyaga kwa nyuma ananiomba msamaha kwamba amenikanyaga bahati mbaya kwa vile alikuwa na haraka huku aiwa anaendelea kwenda kwa mwendo wa haraka na wale tuliopishana nao pia wakaenda na haraka zao mimi muda wote sikujua picha inayochezwa,nilipobaki peke yangu nikawa nafikiria kilichofanyika siyo kitu cha kawaida ndiyo naangalia mfukoni simu hakuna, nikataka kuwakimbilia wale niliopishana nao siwaoni,nataka kumkimbiza aliyenikanyaga kwanyuma akanipita naye kashapotea nika baki naombolezea simu yangu ya laki 5 we acha tu usinikumbushe tena.