Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
785
Reaction score
1,413
Sitatumia maandiko ya Dini Quran wala Bible, labda wataelewa kidogo, maana humu JF nimegundua wapo wengi, unaweza ukajikuta una chati hata na shetani directly, anapotosha

Tuanzie kwenye Civilization na Level ya akili na kufikiri viumbe mbalimbali wapo kwenye level tofauti za civilization na akili. Inaweza kuonekana kupitia namna yao ya maisha.

Mfano Simba wana territory yao wanaweka alama kabisa iwe kuacha kinyesi n.k ila wana mipaka ya utawala na kuna utawala wa simba dume eneo hilo ambapo akiingiliwa na Simba mwingine ambae hakua hapo lazima wapigane vibaya sana hadi moja akubali show.

Tembo pia vilevile kiasi kwamba mwenzao akifa wanahizunika na kuonyesha kuomboleza...

Mchwa pia, wapo wana utawala wao, wana malkia, kuna walinzi kuna wajenzi, na wanajenga haswa, kichuguu kimejengwa kwa ustadi haswa inaonyesha kabisa wana mawasiliano mazuri sana na wanajua wanachokifanya.

Nyuki pia vile vile, wana jenga nyumba yao, sehemu ya kuwekea asali, kuna malkia, kuna wanaolinda eneo, nknk.

Yaani hadi wanavyotengeneza asali kumlinda malkia na kulinda eneo lao, lina onyesha wazi level yao ya kujielewa na level ya mawasiliano ni kubwa kabisa.

wanyama ni wengi ambao tunaweza kuwa tumia kama reference, Sokwe etc.

Hawa viumbe wote, kila mmoja kwa nafasi yake mfano tuchukulie nyuki, wanajiona wana akili(ni kweli wanayo),
wanajiona wanajua mambo mengi na kufikiri logically kwamba huyu ametuchokoza kwaiyo tuji-oganize kushambulia na kujilinda, wanajua kujenga, wanamuheshimu malkia na kumlinda...

ila pia kuna mambo hawajui na hawajui kama hawajui na hawawezi kukuelewa hata ukijaribu kuwaelewesha,
na hautakua hata na intrest ya kuwaelewesha...

Mfano: Je binadamu anaweza kua na interest ya kutaka kumuonyesha nyuki ni jinsi gani binadamu wameendelea kiteknolojia?

Nyuki anaweza kuelewa kwamba binadamu anaweza kuongea na mtu wa marekani kupitia iternet kwamba binadamu anaweza kuwasiliana hivi Jamii Forums kwa id fulani na hawajawai kuonana wala kua na namba ya simu wala kukutana?

Nyuki anaweza kuelewa kwamba hilo bomba linalotoa maji au hiyo taa inayowaka usiku barabarani au nyumbani imetengenezwa na binadamu na sio kwamba ipo tuu... inakazi na bili zinalipwa?

Hayo ni baadhi ya maendeleo ya binadamu na kujaribi kulinganisha uwezo wa akili wa nyuki na binadamu,

Ni dhahiri kwamba hai make sense kwa nyuki, na hatuna interest ya kutaka kumuelewesha

Tumetofautiana kiakili na nyuki kiasi cha kua sisi tunaweza kumuelewa nyuki ila yeye hawezi kutuelewa

Nyuki nae usipo mlinganisha na binadamu, ana akili kubwa tuu na huenda anajiona vilevile binadamu anavyojiona kiakili, na anakiamini kile akili yake inachowaza kumbe ndo akili yake ilipoishia.

Vile vile kwa binadamu anajiona yupo advanced kiakili ambayo ni kweli pia kwa nafasi yake lakini pia na yeye ana limit ambayo akili yake inaishia.

Tunaona tu dunia, jua mwezi, maporomoko na vingine, ni kama tuu nyuki akikutana na taa, bomba la maji, kweli anaona taa inatoa mwanga, bomba linatoa maji...

Ila hajui hasa lile bomba imekuaje lipo pale, au taa imekuaje ipo pale, imewekwa na nani?

Anachojua inatoa mwanga, mechanism nyuma yake je inakuaje inawaka usiku mchana haiwaki? Inakazi gani haswa? Hajui na hana uwezo wa kufatilia kujua.

probably akiona gari anajua ni mojawapo ya viumbe wengine, hajui kama binadamu ndo yupo ndani anaendesha. au anaweza kua analichukulia kwa namna tofauti kabisa. au hata haelewi chochote.

Hiyo ni relation tu ya kuonyesha jinsi akili ya viumbe mbalimbali ina limit yake

Binadamu pia limit ya akili yetu ina limit inapoishia

Mfano ndo unakutana na Mtu anayesema "Mungu Hayupo kwasababu Huwezi kumuona wala kumgusa wala kusikia sauti yake"

Hiyo ni moja wapo ya limit ya akili yetu, ina depend moja kwa moja na milango ya fahamu, masikio macho, pua, ulimi, ngozi...

Anakwambia "jua lili kwepo tuu, na dunia ilikwepo tuu, kwamba kama jua au dunia haiwezekani kuwepo tuu, basi na Mungu hawezekani kuwepo"

Inaonyesha ni jinsi gani akili yetu inafikia limit, kuyaelewa mambo mengine..

Mambo ambayo hatuyajui bado ni mengi ni infinity ♾️, na ningumu hata kuingia akilini haya make sense kwasababu yapo beyond uwezo wa akili.

Kama vilevile tulivyoona kwa mfano wa nyuki, kwamba kumuelezea hata teknolojia yetu hai make sense, kwaajili ya limit yao ya akili.
 
Ukipinga uwepo wa Mungu au shetani inabidi usiamini katika dhana ya ubaya wa jambo lolote au uzuri wa jambo lolote kwa sababu kama uwepo wa Mungu na shetani ni myth basi kudhani jambo fulani ni baya au zuri ni myth, kudhani kwamba ukiua mtu ni jambo baya hiyo ni upotofu maana sababu inayotufanya tusiuane na kama nikileta sababu zangu za kuua inabidi zikubaliwe na ukipinga hizo ni shida zako sio zangu kwa kuwa siamini kama kuua ni jambo baya regardless sababu au bila sababu
 
Mkuu umeelezea vizuri Sanaa, Ila ngoja ni-quote quran kdog ku-summary maelezo yako.

"66.Na mwanadamu husema: je nitakapo kufa ,Ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?

67.Je hakumbuki mwanadamu ya kwamba tulimuumba hapo kabla na Hali hakuwa chochote?

68.Basi naapa na mola wako mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashe'twani Kisha tutawahudhurisha kuizunguka jahannam Hali ya kuwa wamepiga magoti. ...,..... mpaka aliposema Allah عز وجل .
77.Je? umemwona Yule aliyezikufuru(pinga) ishara zetu na akasema:kwa Hakika Mimi nitapewa Mali na wana!.

78.KWANI YEYE AMEPATA KHABARI Za GHAIBU(MAMBO YALIYO JIFICHA KWA MACHO/MASKIO ),AU AMECHUKUA AHADI KWA ARRAHMANI MWINGI WA REHEMA?" Quran(98:66-78).
 
Ukipinga uwepo wa Mungu au shetani inabidi usiamini katika dhana ya ubaya wa jambo lolote au uzuri wa jambo lolote kwa sababu kama uwepo wa Mungu na shetani ni myth basi kudhani jambo fulani ni baya au zuri ni myth, kudhani kwamba ukiua mtu ni jambo baya hiyo ni upotofu maana sababu inayotufanya tusiuane na kama nikileta sababu zangu za kuua inabidi zikubaliwe na ukipinga hizo ni shida zako sio zangu kwa kuwa siamini kama kuua ni jambo baya regardless sababu au bila sababu
ni kweli mkuu📌
 
Mkuu umeelezea vizuri Sanaa, Ila ngoja ni-quote quran kdog ku-summary maelezo yako.

"66.Na mwanadamu husema: je nitakapo kufa ,Ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?

67.Je hakumbuki mwanadamu ya kwamba tulimuumba hapo kabla na Hali hakuwa chochote?

68.Basi naapa na mola wako mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashe'twani Kisha tutawahudhurisha kuizunguka jahannam Hali ya kuwa wamepiga magoti mpaka aliposema Allah عز وجل .
77.Je? umemwona Yule aliyezikufuru(pinga) ishara zetu na akasema:kwa Hakika Mimi nitapewa Mali na wana!.

78.KWANI YEYE AMEPATA KHABARI Za GHAIBU(MAMBO YALIYO JIFICHA KWA MACHO/MASKIO ),AU AMECHUKUA AHADI KWA ARRAHMANI MWINGI WA REHEMA?" Quran(98:66-78).
shukran sana mkuu
 
hadi akili ya binadamu kua na limit ni swala la kuthibitisha ?

ni vitu vingapi binadamu wameshindwa kuvielewa kwa miaka na miaka ?
Unathibitisha vipi wameshindwa kuvielewa?

Au ni kwamba bado utafiti na uchunguzi wa kina haujafanyika kufahamu vitu hivyo?

Watu wangapi walikufa kwa ugonjwa wa malaria kabla dawa za malaria hazijafahamika na kugunduliwa?

Watu wangapi walishindwa kusafiri angani kabla ndege🛫 hazijafanikiwa kuruka?

Si kwamba akili ya binadamu ina limit, Ni kwamba kuna baadhi ya mambo bado hatuyafahamu ila kadiri ya tafiti, uchunguzi na udadisi zinavyo endelea kufanyika tunafahamu vitu vingi na kuondoa hiyo limit unayo idai.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua, ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, uchunguzi na udadisi.

Na si kweli kwamba akili zetu zipo limited.

Maana kuna vitu vingi sana tulikuwa hatuvijui ila leo hii tunavijua.

Kwa hiyo huwezi kusema kwamba akili zetu zilikuwa limited, Ni kwamba utafiti na uchunguzi ulikuwa bado haujafanyika ipasavyo kuleta uvumbuzi.
 
basi nawe kusema Mungu hayupo ni kwasababu bado hujafikia huko,

baada ya hizo tafiti za kina unazo zidai labda wata thibitisha yupo !
 
Back
Top Bottom