Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Ukitaka kuthibitisha gravitational force ipo chukua jiwe rusha angani likiendelea kwenda angani basi gravitational force haipo.

Likirudi chini nenda kasome sayansi uone inavyo sema kisha utathibitisha mwenyewe.
 
Shuhuda za kiungu kama zipi? Gravitational force Ipo maana inaweza kupimwa, we Mungu unamthibitishaje?
 
Fuatilia statistics za France, united kingdom Sweden, norways nk kuhusu population inayoamini dini alafu urudi kuniambia.. ukitoka hapo angalia Korea, china, nk
Missionaries walitokea wapi walioeneza dini Afrika?
 
Anaetetea madai ya uwepo wa kitu ndie anawajibika kutoa uthibitisho au kuelezea logically or scientifically mzee baba. Sasa unasema Mungu yupo bila kuonyesha uthibitisho halafu unataka anaekataa akueleze kutokuwepo kwake.!. Mkuu upo sawa kichwani?
 
Shuhuda za kiungu kama zipi? Gravitational force Ipo maana inaweza kupimwa, we Mungu unamthibitishaje?
Unaaminije kuwa hicho kipimo kinapima gravity? Je hio gravity yenyewe sio dhahania tu kama dhahania nyingine?
 
Science sio Imani, ni kitu halisia, na ndio maana dini na sayansi ni vitu visivyochangamana, sababu dini ni nadharia tu...
Lakini ulisema unaiamini science kwakuwa inathibitisha vitu tangible?

Au umebadili gia
 
Huyo anaepinga uwepo wa mungu ana matatizo makubwa sana. Je jiulize nyumba inaeza ikajijenga ikajiekea bati , tiles, rangi n.k ?? Kama nyumba inakua na designer je sisi viumbe wenye akili, nature and natural selection haiwez kutengeza k2 ambacho kipo perfect, nature is total chaos, ingekua hatuna designer, ungekuta labda tuna mkono mmoja, labda jicho liko tumboni, au uumbaji wetu usingekua perfect, perfection yako wewe fala anayesoma comment yangu ni uthibitisho tosha kwamba Kuna DESIGNER alietengeneza hizi blueprints za Duniani ambaye ndio muumba wetu mungu. Kwa akili zako za kisoda , unaeza kusoma zaidi ili kuthibitisha uwepo wa mungu kwa kubonyeza link hii Has Science Discovered God?
#No malice to anybody
 
Aliyekwambia sayansi ni imani ni nani?

Hebu leta andiko lolote linalosema sayansi ni imani.
Muulize BRAIN BOX yeye kasema anaiamini science kwakuwa inathibitisha vitu tangible

Hebu muulize kwanini anasema anaiamini science?
 
Missionaries walitokea wapi walioeneza dini Afrika?
Uko unapoelekea unataka tukufundishe historia Sasa, ni hivi dini ya kikristo ilisambaa ulaya kupitia utawala wa Rumi, kumbuka kipindi icho Rumi ndo lilikuwa taifa lenye nguvu Duniani, alikuwepo mfalme Constantine ambae mwanzoni alikuwa mpagani, baadae akabadilsha dini na kuwa mkristo na kutoa amri taifa lake liwe la kikristo.. ukristo ukaendelea kusambaa kama utamaduni wa taifa kubwa unavosambaa kama lugha, uvaaji na kadhalika vinavoweza kusambaa.
 
Sasa uwepo wa gravitational force unahusiana nn na kutokula nguruwe?
Wewe una kinzana na baadhi ya dini ila unaamini kuwa Mungu yupo kama ilivyokuwepo gravity shida tu hayo ni maneno ya dhahania ambayo yanahitaji uthibitisho ila kuwa Mungu yupo unaamini hilo
 
Lakini ulisema unaiamini science kwakuwa inathibitisha vitu tangible?

Au umebadili gia
Nina iamini sayansi ndio, kwa sababu imethibitisha vitu, siwezi kumuamini Mungu maana hawezi kuthibitika
 
Mungu kajijenga?
 
Aliyekwambia sayansi ni imani ni nani?

Hebu leta andiko lolote linalosema sayansi ni imani.
Kwaiyo nikileta andiko utaamini? Kumbe nawewe unaamini maandiko?

Na vipi kama hayo maandiko ni ya kutunga?
 
Na uyo Mungu yeye ameumbwa na nani?
 
Wewe una kinzana na baadhi ya dini ila unaamini kuwa Mungu yupo kama ilivyokuwepo gravity shida tu hayo ni maneno ya dhahania ambayo yanahitaji uthibitisho ila kuwa Mungu yupo unaamini hilo
Siamini juu ya uwepo wa Mungu kaka, kama unaweza kunithibitishia uwepo wake, nitaanza kumuamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…