Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Ukitaka kuthibitisha gravitational force ipo chukua jiwe rusha angani likiendelea kwenda angani basi gravitational force haipo.

Likirudi chini nenda kasome sayansi uone inavyo sema kisha utathibitisha mwenyewe.
Kama haumini uwepo wa Mungu unakuwa sawa na mbumbu tu

Kwani Sayansi ni Nini?

Maana ninachojua Mimi Sayansi ni kujifunza jinsi gani Mungu kaumba ulimwengu na viumbe vyake

BIOLOGY
binadamu anajifunza jinsi gani Mungu kaumba viumbe hai hakuna kiumbe chochote kilichoumbwa na mwanasayansi zaidi ya kujifunza hivyo alivyovikuta

CHEMISTRY
Binadamu anajifunza jinsi gani Mungu kaumba chemical reaction hakuna binadamu yoyote aliumba atoms zaidi ya kujifunza hizo alizozikuta

GEOGRAPHY
Binadamu anajifunza jinsi gani Mungu kaumba ulimwengu Nyota na Sayari
Hakuna binadamu yoyote aliyeumba Sayari zaidi ya kujifunza hizo alizozikuta

Na bado Kuna mambo mengi yapo hapa ulimwenguni na hao wanasayansi hawayajui Kwa sababu upeo wao ni wakibinadamu mtoa mada amesema una limit

Ni mjinga pekee anayeweza kuutenganisha Sayansi na kazi za Mungu
 
Kwaiyo nikileta andiko utaamini? Kumbe nawewe unaamini maandiko?
Ukileta andiko na hicho kilichomo na kinacho elezewa kwenye hilo andiko kinathibitishika kweli kipo, Andiko hilo litakuwa la ukweli na uhakika.
Na vipi kama hayo maandiko ni ya kutunga?
Ukileta andiko lisilo na uthibitisho wowote ule wa hicho kilichomo na kinacho elezewa kwenye andiko hilo,

Kitu hicho na andiko hilo litakuwa ni uongo sawa na hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.
 
Unarukia kusema Mungu kaumba ulimwengu na viumbe vyake, Halafu hujathibitisha uwepo wa huyo Mungu?

Huoni kwamba unafosi mawazo yako uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule?

Thibitisha kwanza huyo Mungu yupo, Kisha ndio ueleze namna gani aliumba ulimwengu na viumbe?

Unarukia kuhesabu mbili badala ya kuanza na moja!!
 
Ntakuja kukujibu hilo, kwanza jielimishe vzuri nliweka link kwenye comment yangu. Ukishakua na maarifa ndio ntaeza kukuelezea vyema lkn saiv Bado ww mweupe kabisa
Sawa kaka, iyo article Yako nimeisoma yote, lakini hakuna sehemu wamethibitisha kuwa Mungu yupo.
 
Hapa umedanganya, ila Cha msingi usikwepeshe mada, thibitisha uwepo wa uyo Mungu.
 
Soma page zote saba. Uthibitisho sio mungu , ni Designer ambaye sisi tunamuita Mungu
Nimeisoma yote, naona ni baadhi ya wanasayansi Wana kiri kuwepo kwa Mungu, lakini kiimani bila evidence
 
Soma page zote saba. Uthibitisho sio mungu , ni Designer ambaye sisi tunamuita Mungu
Wanasema kwa mfano, kuwepo kwa DNA Kunaonesha Kuna Mungu, lakin hawajotoa uthibitisho kuwa uyo Mungu yupo, wame speculate tu
 
Hakuna mtu anaye pinga uwepo wa Mungu. Watu wanapinga vitabu fake vya dini. Ambavyo vinadanganya watu kuwa vilishushwa na Mungu wakati viliandikwa na watu tu kama mimi na wewe. Mungu anawasiliana na kila binadamu bila kujari dini ya mtu . MUNGU HAJUI ISLAMA WALA UKIRISTO. TUKIKUBALIANA KUWA VITABU VYA DINI KUWA NI ULAGHAI TU. KAMA TUKIKUBALIANA KWA HILO THEN TUNAWEZA KUBISHANA KUHUSU UWEPO WA MUNGU.
 
Anaetetea madai ya uwepo wa kitu ndie anawajibika kutoa uthibitisho au kuelezea logically or scientifically mzee baba. Sasa unasema Mungu yupo bila kuonyesha uthibitisho halafu unataka anaekataa akueleze kutokuwepo kwake.!. Mkuu upo sawa kichwani?
Mkuu Elewa kwanza basi,
Mimi sitaki unithibitishie kama hayupo, nataka unielezee logically hadi ukafikia conclusion hayupo. Otherwise uko tu brainwashed na ideas za mtu anayefikiria mungu hayupo na wewe ukalibeba zima zima kama mtu asiye na ubongo
 
Afu pia utuambie ni Mungu gani unamuongelea hapa Allah, Yawhew, Zeus, Sangoma, Vishnu au Warumbe. Kuwa specific.
Kuna miungu zaidi ya 4000 Duniani
That's not the topic of today, save that argument for the other day, unless kama unakiri Mungu yupo tuendelee na argument nyingine ya kumdescribe yeye mwenyewe
 
So, wote mnakubali kama Mungu yupo ila dini ndo mnazikataa?? Labda mnieleze vizuri hapa, ukute tunabishana alafu hakuna mada
 
Uwepo wako wewe hapa Duniani pia ni Moja ya uthibitisho kama Mungu yupo otherwise usema ilikuwaje Hadi wewe Leo hii upo hapa Duniani
 
Mkuu Elewa kwanza basi,
Mimi sitaki unithibitishie kama hayupo, nataka unielezee logically hadi ukafikia conclusion hayupo. Otherwise uko tu brainwashed na ideas za mtu anayefikiria mungu hayupo na wewe ukalibeba zima zima kama mtu asiye na ubongo
Hakuna popote ambapo ambapo nimesema Mungu hayupo. Kwa lugha rahisi tuseme nipo neutral.
 
Hakuna mtu anaye pinga uwepo wa Mungu.
Mimi hapa napinga uwepo wa huyo Mungu.

Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Watu wanahangaika sana kumuongelea na kumuelezea huyo Mungu kwa vile hajawahi kuwepo, hayupo na wala hatakaa awepo kujidhihirisha na kujiongelea mwenyewe yeye kama yeye.
 
So, wote mnakubali kama Mungu yupo ila dini ndo mnazikataa??
Utakubalije kitu ambacho hakina uthibitisho zaidi ya madai tu?

Ukidai Mungu yupo mthibitishe yupo, kama huwezi kuthibitisha Mungu yupo, Ni kwamba hayupo.

Sasa ninyi waamini Mungu mnaleta madai ya uwepo wa Mungu halafu uthibitisho hamna, Mnataka sisi ambao hatujui huyo Mungu wenu ni nini tuwathibitishie madai yenu!


Labda mnieleze vizuri hapa, ukute tunabishana alafu hakuna mada
Mlio ibua madai ya uwepo wa Mungu ni nyie Theists, Sasa thibitisheni hoja zenu na madai yenu.

Sisi Atheists hatumjui huyo Mungu ndio maana tunasema hayupo.

Leteni uthibitisho wa uwepo wa Mungu huyo tumjue yupo.

As simple as that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…