Uzi maalum kwa wastaafu kupeana changamoto mbalimbali na connection

Uzi maalum kwa wastaafu kupeana changamoto mbalimbali na connection

Wastaafu hebu tukutane hapa tupeane taarifa za kupambana mtaani, changamoto mbalimbali na connection mbalimbali na kielekezana na mbalimbali kukabiliana na maisha ya mtaani
Hakuna changamoto mambo yote ni shwari ikiwa umejipanga vizuri.

Ndiyo muda wako wa kupumzika na kutembea nchi mbali mbali kujionea dunia
 
Daah nipo chini ya mwembe nasikiliza BBC hapa...

"Sababu ya vita ni Mmarekani" 🙄🙄
 
Ila mafao yanaisha haraka sanaaaaaa haswa ukiwa na ATM card, mimi naichukia sana ATM card maana unaenda kutoa tu kila zikiisha unaenda kumbe na kule kwenye acc ndio zinaondoka hazirudi tena.....

Kuna siku nilienda bank nikatoa nyingi basi nikawa nazo ndani nachomoa mdogo mdogo kuja kuangalia bahasha ipo tupu yaaani mpk nikaichana ili kuhakiki maana nikawa siamini aiseeee hela inaenda
Aiseee,nimecheka kisenge yani [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mzee mwenzangu utelezi unazidi kuchosha mwili na kumaliza pensheni.

Jenga nyumba town za mzunguko pangisha kisha urudi kijijini kujenga mjengo, kufuga, kilimo, duka la kupotezea muda.

Hutakiwi kuwa na stress utelezi waweza leta magonjwa pesa wazitafune wengine.
Mstaafu hatakiwi kuanza ujenzi mpya
 
Back
Top Bottom