Hello ndugu, nakushukuru kwa kuja na uzi huu mana kuna wengi tunataman kuagiza gar toka nje lakin utaratibu na hasa zaid mchanganuo wa gharama had gar inakufkia imekuwa changamoto xanaaa..... Pia ningetaman kujua kwann gharama za TRA huwa kubwa kias cha sawa au zaid ya bei ya gari uliloagiza?!?
Sasa kwa upande wng nataman kuagiza gari aina ya Noah old model SR40.... Kwaajil ya familia.....naomba maelekezo na mchanganui kwa ujumla.......
Asante ndugu.... Nawasilisha kwako.....
Hello,
Ahsante kushukuru.
kuhusiana na kwanini TRA hua wanatoza kiasi ambacho huonekana kama ni sawa ama zaidi na bei ya kununulia gari yenyewe. Kwa majibu ya kina kabisa, nadhani wao (TRA) Ndio wanaweza kuyatoa na kwa ufafanuzi mkubwa zaidi.
Kuhusiana na Noah,
naomba nikupe mfano halisi wenye michanganuo.
(kwenye link hiyo hapo juu, ni toyota Noah SR40 )
Bei ya manunuzi hadi kuifikisha bandari ya Dar es salaam ni $4,4497 (TZS 10,792,800 )
Ushuru wake ni TZS 6,553,000/=
(
https://gateway.tra.go.tz/umvvs/Umvvc_result)
Ambapo itakuja jumla ya TZS 17,345,800/=
Unapaswa kuwa na TZS 800,000/=
ambayo ita-cover
- Port Charges
- Shipping Line
- : Walfage
- Agent Fee (gharama za agant wako atakae kutolea gari lako bandarini)
n.k
ambapo jumla itakua 18,145,800/=
usisahau kuhusiana na bima utahitajika gari yako kuikatia bima.
comprehensive watakutoza TZS 750,000/=
Jumla kuu TZS 18,895,800/= Hadi barabarani /mikononi mwako
bei sawa na ALPHARD