UZI MAALUM: Simba SC na Yanga SC; Utani , kumbukumbu na uhalisia wao!

UZI MAALUM: Simba SC na Yanga SC; Utani , kumbukumbu na uhalisia wao!

njeeseka

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
1,373
Reaction score
983
Homa ya Kariakoo Dab ndio hiyoooooo.

Mbali na timu hizi kuwa ndio kongwe nchini, pia ndizo zenye washabiki wengi kwa sasa nchini Tanzania na nje ya nchi kama tulivyoona siku za hivi karibuni huko Burundi na Rwanda kuna mashabiki wa timu hizi.

Pamoja na yote yanayosemwa kati ya Simba na Yanga, kuna vitu vinafanyika nje ya dimba kabla ya kipenga kupulizwa. Hapo utasikia kambi imewekwa sehemu salama, mara ooh nani atakuwa wa kwanza kuingia uwanjani.

Wakati mwingine marefa nao ki ubinadamu utakuwa na yeye ni mpenzi wa either Simba au Yanga. Kuna siku nilishuhudia mechi moja yaani refa alishindwa tu kusaidia pasi pindi mpira unapomfuata..achana na hizi timu, ni Ma jayant kwa kweli.

Hata wachezaji wakichukuliwa na hizi timu wanajisikia raha saaaaana mfano Tambwe alishawahi kusema, hakuna raha anayoipata zaidi ya kucheza mechi kati ya hizi timu mbili.

Kuna mengi ya kuongea ila nawaachia ukumbi mtiririke, maana pande huu kuna Ajibu na upande ule kuna Okwi. Mmmh kweli wakutanapo mafahali wawili nyasi hung'oka...ingawa safari hii kuna nyasi bandia..ha ha haaa
 
Nasikia leo saa 2 usiku Mkemi na Manara watapambana kupitia azam tv
 
Kwa hiyo utaratibu ni ule ule wa kadi kama uwanja wa Taifa?
Nilivyosikia, utaratibu ni uleule na pia km ukichelewa tiketi hazitauzwa siku hiyo maana zinaweza kwisha kwani kauwanja kinyewe ni uhuru.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Nilivyosikia, utaratibu ni uleule na pia km ukichelewa tiketi hazitauzwa siku hiyo maana zinaweza kwisha kwani kauwanja kinyewe ni uhuru.

Toka uwanja wa Taifa uzinduliwe siku ile tunapigwa na Msumbiji sijawahi kucheki game tena Uwanja wa Uhuru, maana Taifa ni kama Anfield raha yake.
 
Kwa hiyo utaratibu ni ule ule wa kadi kama uwanja wa Taifa?
IMG_20171025_161058.jpg
 
Toka uwanja wa Taifa uzinduliwe siku ile tunapigwa na Msumbiji sijawahi kucheki game tena Uwanja wa Uhuru, maana Taifa ni kama Anfield raha yake.
Uwanja wa Taifa ulizinduliwa na Stars Vs Uganda, ikapigwa gemu ya usiku na Stars ilishinda 1 kupitia ABDI KASSIM BABY ballack wa Unguja. Umeme ulikatika for several minutes huku tukipiga mayowe wanazindikaaaaa. So ukisema ulizinduliwa na Msumbiji sijakupata mkuu
 
Back
Top Bottom