MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Hizi ni tabia zinakufanya uendelee kuwa fukara. Mtajazia nilizosahau.
1. Kutojiambia ukweli kuhusu makosa yako na kuchukua hatua badala yake unatafuta visingizio na kujifariji kipuuzi.
2. Kuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chako. Acha tamaa. Kama uwezo wako ni dagaa kwa sasa usilazimishe kula kuku. Hata nyie mnaosomesha watoto shule za bei mbaya huku kipato hakifiki hata 2m kwa mwezi acheni hiyo tabia.
3. Pamoja na kwamba kipato chako hakitoshi kukulipia mahitaji ya lazima kibinadamu ila hufanyi jitihada zozote kutafuta chanzo kingine hata kidogo cha mapato.
4. Kuchagua kazi. Unaona kuuza maandazi ni ya kina mama watu wazima ambao hawajasoma kumbe ni kazi inayowapatia pesa kibao hadi kufanya maendeleo. Binafsi huwa naamka mapema sana na kutengeneza vitafunwa ninavyopeleka madukani. Hadi kufika muda wa kwenda kazini kwangu tayari nakuwa nimesambaza. Hivyo vitafunwa vinanipa angalau 50k kila siku.
5. Kuwa na wapenzi wengi wanaokugharimu pesa nyingi. vocha, saluni, usafiri nk. Hata mpenzi mmoja mpumbavu anaweza kukufilisi.
6. UOGA. UMASKINI NA UOGA NI NDUGU WA DAMU. Kwa sisi wakristo kwenye biblia tumeona jinsi gani Mungu alikuwa mbali na waoga. Hajawahi fanya kazi na mtu muoga. Musa aliua mmisri. Yakobo alipigana na malaika. Yona alimgomea Mungu kwenda Ninawi. ila wote hao Mungu aliwaona wanafaa kwa kazi yake. Kwa hiyo ndugu yangu acha uoga na chukua hatua ya kujikwamua. Mtu legelege ni chukizo kwa Mungu.
7. Kuoa single mama fukara kama wewe. Jomba kama umeamua kuoa single mama chukua mwenye mpunga mrefu ili usije kuanza kulipia bills zake na mtoto wake.
8. Uzembe kwenye mawasiliano. Hujibu messages wala simu kwa haraka. Kwenye huu ulimwengu wa leo jitahidi kupatikana kwenye means zote za mawasiliano.
9. Kudhani mwanasiasa kama mbunge ndo atakutatulia changamoto zako. Utasubiri sana mkuu.
10. Kumpa nabii, mchungaji au mtume kanisani zile sadaka za kujimaliza.