Uzi maalum wa kupata connection za ajira na machimbo mengine

Uzi maalum wa kupata connection za ajira na machimbo mengine

Babumawe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
2,556
Reaction score
2,571
Hivi sasa kutafuta ajira Tanzania ni kazi ngumu sana.

Ukweli ni kwamba kuna watu wengi zaidi wanatafuta ajira lakini wanakosa connection ya watu either hafahamiki na watu wenye potential au hata baadhi ya machimbo ya kwenda kujishikiza hayajui.

Unakuta mtu kamaliza chuo hana hata pa kuanzia au mtu katoka village kaja town hana pa kuanzia na hii inatokana na kukosa watu wa kumdirect either kwenda sehemu fulani au kumuweka sehemu Fulani.

Naamini hapa JF kuna watu mashuhuri ambao wana roho ya huruma na wapo kwenye idara tofauti na kuna wengine wanataka kusaidia wengine ila hawapati wanaojitokeza sasa naamini huu utakuwa Uzi kwa wale wote ambao wako sehemu fulani na wanataka kusaidia wengine na wale wote wanaotaka msaada kujitokeza ili kuonekana humu na ikiwezekana kupata connection.
 
Ni wazo jema, je wewe upo kwenye ajira na unaongelea wasio na ajira? Au nawe ni muhanga mwenzetu wa ajira.
 
Sasa baada ya maelezo yako yote, nini dhamira/malengo yako?

Manaa ni kama hujamaliza ulichokuwa unataka kukizungumza!
 
"Naona watalaam wako kazini kutafuta kuwajua wanazi wa JF" Alisikika mtu mmoja baada ya kusoma uzi huu
 
"Naona watalaam wako kazini kutafuta kuwajua wanazi wa JF" Alisikika mtu mmoja baada ya kusoma uzi huu
Hapana kuna watu wanakosa connection halafu maisha tough aisee sasa viuzi kama hivi vinaweza kuwanufaisha.
 
Back
Top Bottom