Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

*UJUMBE WA LEO*

*1 SAMWELI 9: 17*

*"Hata Samweli alipomwona Sauli, BWANA akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu."*

Kupotea kwa n'gombe wa babaye Sauli, ndani yake ulifichika mpango wa Mungu wa kumfikisha Sauli kwa Samweli ili aandaliwe kuwa mfalme wa Israeli.

Mpendwa, usihesabu kila jambo gumu au hasara fulani unayoipata kuwa ni mkosi kwako. Yapo mengine yanayokutokea ili kukuelekeza katika njia bora zaidi ya mpango mzuri wa Mungu juu ya maisha yako. Usiishi kwa kujuta na kukata tamaa. Mshukuru Mungu na usonge mbele. Anayowaza Mungu kwa ajili yako kila wakati ni mema sana. Simama tu katika shauri lake, mtumaini Yeye peke yake.

*MUNGU AKUBARIKI*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameen Mtumishi wa Mungu na usiku utupatie mstar wa kulala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…