Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_3114.JPG
 
Muimbaji huyo ambaye ni ndugu na Alikiba na chini ya Kiba Squared walishatoa hit song kama Kidebe, amesema Alikiba kwa sasa yupo nje ya nchi na akirejea ngoma mpya itadondoka. “Alikiba kwa sasa yupo nchini Kenya amekwenda kufanya jambo na gavana wa Mombasa Joho ila nadhani hawezi kumaliza wiki atarudi nchini, kwa hiyo nachojua mimi yeye yupo kwenye mchakato wa kuachia ngoma mpya hivyo naamini akisharudi kila kitu kitakuwa sawa,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio. Alikiba kwa sasa ana muda wa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoe wimbo wa Aje uliotoka May 19 mwaka jana kitu ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na mashabiki wake. .
 
Jumamosi ijayo ya tarehe 5 mwezi Agosti 2017, Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museven wataweka jiwe la Msingi kuzindua mradi wa Bomba la kusafirishia mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania. Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa na uwekezaji wake unagharimu Dola Bilioni 3.5 ambazo ni sawa na Trilioni 8 za Kitanzania.
 
Msanii wa Bongo Fleva ambaye haishiwi vituko, Harmorapa amekunwa na utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli wa kubana fedha kitu ambacho kimewafanya watanzania kutumia pesa kwa nidhamu. Harmorapa amesema kipindi hiki cha awamu ya Rais Magufuli kimewafanya watanzania kuithamini pesa ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi yasiyo na ulazima kitu ambacho ni tofauti kabisa na kipindi cha nyuma. “Kwanza mimi nimpe tu pongezi kwa sababu amefanya watu wengi sana wajue kuhangaika na wajue kufanya kazi tofauti na kipindi cha nyuma watu walikuwa wazembe”,amesema Harmorapa baada ya kuulizwa swali la kuhoji utendaji kazi wa Rais Magufuli kwenye kipindi cha Twenzetu cha Times FM. Hata hivyo, Harmorapa amesema awamu hii ya tano Serikali imekuwa ikihimiza sana vijana kufanya kazi kuliko kuendekeza starehe kitu ambacho kimewafanya vijana wengi kujituma na kupata molali ya kufanya kazi. .
 
Back
Top Bottom