Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nimepita kwenye kichaka na kukutana na taswira hii ya kufikirisha. Nyuki na nzi wote wametuwa kwenye shada moja la mauwa. Nikajisemea kuwa hatimaye nyuki huyu ataondoka hapa akatumie madini aliyoyakuta kutengenezea asali, na nzi atatumia makinikia kuunda vimelea vya maradhi. Nikajifunza kuwa kwenye maisha, mafanikio hayapo tu kwenye namna fursa ikujiavyo, bali yamo zaidi kwenye namna uitumiavyo. Wahenga walisema: "ukupigao ndio ukufunzao!"
19961471_10155507869994655_6411219732195618553_n.jpg
Word
 
Enzi zangu, kurumbiza huyu angelipatwa na ya mbuzi aliyeangukia kwa muuza supu. Ningemfunga uzi na mwenzake kisha wakaanza kuvutana hewani huku nacheka. Michezo mingine ya kitoto ni ya kikatili kwa viumbe hai wenzetu, Wallah. [HASHTAG]#RIP[/HASHTAG] kwa kurumbiza wote mulioangukia mikononi mwaangu. Tusameheane. Ulikuwa utoto tu.
19958914_10155501792189655_7297602892919971512_n.jpg
 
Akasimama akasema; "Mafisadi wananiogopa! Nitawashughulikia! Wajiandae!"

Nao mafisadi waliposikia, wakajiandaa, wala wasiwape wazee wa sheria SABABU ya kuwashitaki. Wazee wa sheria wakaliomba baraza liwaachie huru wale ambao mwalimu alisema washughulikiwe! Naye mwalimu alipopelekewa habari zile akawakemea sana wasiwaambie watu wa vijijini....

Wale waliomwamini walipoona mambo hayo, wakapatwa na shaka, wakauma meno yao wakilaumiana wao kwa wao kwa kumfanya mfalme wao. Nao wakaulizana, "Imekuwaje jambo hili?" Na yule asiyeamini alikuwa amesimama karibu nao, akajibu akawaambia; "Je, ninyi peke yenu ni wageni huku Yerusalemu? Je hamjui mambo ya 'mviringo mviringo' yanayoendelea siku hizi?"
Wakainamisha nyuso zao wasiweze kumjibu. Naye akaondoka akaenda zake mjini."

Kiki 3:18-21
 
Back
Top Bottom