Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtori ni chakula maarufu sana kwa watu wa kaskazini huko hasa hasa mkoa wa Kilimanjaro. Na kwa sasa maeneo ya mjini mtori umekuwa unanywewa sana mida ya asubuhi kama kifungua kinywa. Sasa leo nakuelezea namna ya kupika mtori mzuri na mtamu.
 
JINSI YA KUPIKA

Kwanza anza na kuikata kata nyama na kuichemsha hadi kuiva kabisa. Wakati wa kuchemsha nyama weka chumvi kidogo na majani ya Bay na iwe na maji ili kupata supu ya kutosha kutengeneza mtori wako. Kuchemka kwa nyama hadi kuiva mda utatengemea namna unayochemsha
 
Chukua chombo kingine ambacho sasa ndio kitatumika kupika mtori ivo kisiwe kidogo sana. Weka katika moto ongeza mafuta kisha weka kitunguu swaumu kikaange kidogo tu kisha weka vitunguu maji na karoti (na mahanjumati masala kama ipo) endelea kuvikaanga kwa muda kama daki 2-3 kisha weka ndizi koroga kidogo ili kuivisha ongeza ile supu ya nyama kidogo. Ivisha kwa dakika 10 – 15 hadi ndizi ziwe zimelainika ila supu ipungue.
 
Ukiona zimelainika vema anza kuongeza ile supu ya nyama kupata ulaini uupendao.
Baada ya kuupata ulaini mzuri wa mtori weka zile nyama kisha rudisha jikoni vichemke pamoja kwa dakia 3-5
Baada ya hapo pishi la Mtori lipo tayari , pakua na kufurahia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…