Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1.Kusoma ndiyo njia kuu ya kujifunza

Umuhimu wa kusoma katika maisha ya binadamu huanzia tangu anapokuwa mtoto shuleni na kuendelea hadi anapokuwa mtu mzima. Ni dhahiri kuwa, wanafunzi wenye ustadi katika kusoma na wanasoma zaidi ndiyo wenye maendeleo mazuri masomoni na wanaofaulu mitihani.
 
Nakumbuka katika miaka ya themanini na tisini nchini Tanzania watu waliokuwa wakisoma vitabu na magazeti walikuwa ni maofisa na wasomi. Siku hizi watu wengi wa aina mbalimbali kama vile wamachinga, walinzi, maman’tilie, wahudumu, madereva, makuli na hata kinamama wa nyumbani wanasoma sana magazeti.
 
Manufaa ya kusoma hayaishii masomoni bali huendelea hadi katika utu uzima. Kadiri mtu anavyokuwa na uwezo mkubwa wa kusoma katika maisha, ndivyo kadri anavyojiongezea fursa ya kupata kazi nzuri. Sio hivyo tu, bali ndivyo kadri anavyoweza kuifanya kazi yake vizuri zaidi.
 
Taarifa hizo muhimu ungeweza kuzipata tu kwa kusoma aina mbalimbali za machapisho kama vile vitabu, majarida na magazeti na vitu vingine kama nyaraka, makabrasha na hati za miongozo mbalimbali. Ulimwengu wa sasa unapitia katika maendeleo makubwa ya mbinu, zana na vifaa vya kufanyia kazi. Mabadiliko haya yanayotokana na sayansi na teknolojia yanakwenda kasi kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya binadamu. Njia moja kuu ya kila mtu kuha
 
Back
Top Bottom