Dk Mavura aliongeza kuwa siyo watu wanaosinzia kwa muda mrefu mchana peke yao waliopo kwenye hatari hiyo ya kupata kisukari aina ya pili bali hata wale ambao hukaa muda mwingi au kutembelea sana gari na kukosa muda wa kufanya mazoezi kwa muda mrefu.
Kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na maumivu ni miongoni mwa dalili za maambukizi kwenye njia ya mkojo au UTI. Baadhi ya wagonjwa huhisi kichefuchefu, wengine hutapika.
Zipo dalili nyingi za maradhi haya. Homa, mkojo kuwa mwekundu usio na harufu ya kawaida, pia uchovu wa mara kwa mara na maumivu chini ya mgongo ni dalili nyingine ambazo hujitokeza.
Mfumo wa mkojo unaundwa na figo na ureta mbili, kibofu pamoja na urethra. Binadamu wote wana vitu hivyo ingawa ipo tofauti ya mfumo huu kati ya wanawake na wanaume.
Tofauti hiyo ni kwamba, wanawake huwa na urethra fupi wakilinganishwa na wanaume. Kutokana na ufupi wa urethra, wanawake wapo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi haya kuliko wanaume.
Takwimu zinaonyesha takriban watu milioni 150 duniani kote, hupata maambukizi kwenye njia ya mkojo, wanawake wakiongoza hasa wenye umri kati ya miaka 16 na 35. Wanawake hupata maambukizi haya mara nne zaidi ya wanaume.
Watoto pia ni waathirika wa maambukizi haya. Inaelezwa kwamba, asilimia 10 ya watoto hupata maambukizi haya kila mwaka. Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa na walio chini ya miezi mitatu wapo kwenye hatari hii na wa kike chini ya mwaka mmoja.

Bakteria wanaelezwa kuwa chanzo kikuu cha maambukizi. Bakteria aina ya escherichia coli wanaelezwa kusababisha maradhi haya kwa kati ya asilimia 80 mpaka 85 na wale wa staphylococci kwa asilimia tano mpaka 10. Ni mara chache virusi au fangasi husabababisha UTI.

Bakteria aina ya staphylococcus saprophyticus husababisha UTI kwa watoto na wanawake waliovunja ungo au waliopo kwenye uhusiano wa ndoa. Clamydia trachomatis na E.coli huchangia kwani huweza kusababisha UTI ndani ya saa 12 mpaka 72 baada ya kufanya tendo la ndoa.
Ugonjwa huu pia huweza kusababishwa na mawe yaliyopo kwenye figo (nephrolithiasis) ambayo huongeza msongamano wa njia ya mkojo hivyo kuvifanya vijidudu vya maradhi vizaliane kwa urahisi.
Tezi dume nalo ni miongoni mwa vitu vinavyorahisisha maambukizi ya njia ya mkojo. Kuvimba kwa tezi hili husababisha kufungwa kwa njia hivyo mkojo kukaa kwa muda mrefu kiasi cha bakteria kuzaliana na kusababisha madhara kwa mgonjwa.
Ugonjwa wa kisukari pia huchochea maambukizi ya UTI kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachokuwapo katika figo na kibofu kwa muda mrefu ambacho huchangia bakteria kuzaliana na kusababisha ugonjwa.