WATU KUMI MASHUHURI WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI (Wamo John Kennedy, Martin Luther King, 2pac Na Wengine)
1.JOHN F KENNEDY (JFK)
Alikuwa raisi wa 35 wa marekani aliuwa November 22 mwaka 1963 akiwa raisi wa nne kuuawa kwa kupigwa risasi katika historia ya marekani. Akiwa na mkewe, kwenye gari la wazi akitoka kwenye hotuba Alipigwa risasi tatu .Mpaka leo hakuna jibu la moja kwa moja juu ya nani aliyehusika kumuua JFK japokuwa Lee Harvey Oswald ndiye aliehusishwa na mauaji hayo.Lee Harvey Oswald nae aliuawa na raia mmoja (Jack Ruby) siku mbili tu baadae alipokuwa akipelekwa rumande. Cha ajabu ni kwamba, John kennedy, Lee Harvey Oswald, na raia aliyemuua Oswald, wote walifia katika hospitali ya Parkland Memorial Hospital kwa nyakati tofauti. Mdogo wa JFK aliyeitwa Robert F. Kennedy nae aliuawa mwaka 1968 (alikuwa anawania uraisi wa marekani)