Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umri: Uwezekano wa kupata saratani hii huendana na umri wa mtu. Kadri umri wa mtu unavyoongezeka ndivyo pia uwezekano wa kupata saratani hii unavyozidi kuwa mkubwa. Wanawake walio na umri wa kuanzia miaka 50 wapo kwenye hatari kubwa (mara 2 au 3 zaidi) kuliko walio na umri wa miaka 45.
 
Uasili wa mtu (ethnicity): Saratani ya matiti hutokea zaidi kwa wanawake Wazungu kuliko wanawake wa Kiafrika au wenye asili ya Afrika (weusi).

Uzazi: Wanawake ambao hawajazaa au kunyonyesha wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti. Wanawake wanaopata ujauzito kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 nao pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…