Bill Gates katoa milioni 500 yupo zake anakula wali maharage, wewe ndugu yangu unatoa 1,500 kwa muuza chipsi unamimina tomato kama unachangia damu, unaondoka na pilipili na unaomba ufungiwe kachumbari huku unapiga kelele "NIMETOA HELA YANGU HAPA NAOMBA TUHESHIMIANEEE TAFADHALI NIMEKUJA WA KWANZA WE UNAHUDUMIA TU WATU WENGINE". Kwenye harusi sasa ukichangia elf 30 unataka kula kila kitu kuanzia kuku hadi matango na unabaki mpaka mwisho uombe keki ya wakwe na kuchukua chakula cha mbwa