UWEZO WA MWAROBAINI KATIKA KUTIBU MAGONJWA YA AINA MBALIMBALI
Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali.
Inaaminika kuwa mti huu asili yake ni India na Burma . Mwarobaini hustawi zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame. Nchini Tanzania, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini.
Mti huu umetumika kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu pamoja na wanyama. Mfano, inaaminika kuwa
kwa binadamu mti huu husaidia kutibu matatizo ya mmeng’enyo wa chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya
ngozi, malaria, fangasi, n.k.
Hali kadhalika mti wa mwarobaini umekuwa maarufu sana katika kutibu mifugo. Hii ikiwa ni wanyama pamoja na ndege.
Dawa ya mwarobaini ina uwezo wa kuua aina mia mbili (200) za wadudu wanaopatikana duniani kote, huku kwa nchi za Afrika ukiwa na uwezo wa kuua aina 50 za wadudu. Dawa hii haidhuru wala kuua wadudu rafiki.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.