Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Idadi kubwa zaidi ya watu wanazidi kupatwa au wanategemewa kupatwa na aina fulani fulani za mifadhaiko. Baadhi ya aina za mifadhaiko ni hali za asili katika hatua za maendeleo na kukua kwa mtu.

Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu uwezo wao ni mdogo kushughurika na woga, wasiwasi na hamaki zinazohusiana na mifadhaiko. Kwa bahati mbaya tena wanapotafuta msaada wa kitaaluma, wanapewa aina fulani za madawa.
 
Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !

Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara wote duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.
 
Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo hasi katika afya ya mwili, pia wasiwasi na hofu ya maisha huweza kuleta magonjwa yanayoweza kuuwa kabisa sawa sawa na inavyotokea pia kwa magonjwa yale yatokanayo na lishe dhaifu.

Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.
 
Back
Top Bottom