Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Masaji ya mwili itakufanyia ujisikie vizuri kimwili na kiakili pia. Kwa kazi hii unaweza kutumia mafuta ya nazi ua ya ufuta au ya karafuu kwa matokeo mazuri zaidi.

Mara moja moja katika wiki pata nafasi ya kupata huduma hii ili kuzuia na kukabiliana na tatizo la msongo wa mawazo (stress).
 
11. Kahawa

Kahawa inao uwezo pia wa kukufanya ujisikie vizuri na hivyo kuondoa msongo wa mawazo. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa asubuhi ikiwa unakabiliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili.

Hata hivyo kuwa makini, kunywa kahawa kupita kiasi kunaweza kukupelekea ukapatwa na mfadhaiko zaidi sababu kahawa ina kaffeina ndani yake ambayo ni dawa ya kulevya kundi la madawa ya kulevya yanayosisimua akili (stimulants drugs).
 
12. Mafuta ya habbat soda

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa katika kudhibiti tabia za kuhamaki na wasiwasi na hivyo kukuwezesha kujisikia vizuri kila mara. Na utaona matokeo haya baada ya matumizi ya habbat soda kwa siku 30 hivi.

Tafiti kadhaa zimeonyesha watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda wanakuwa ni watu wenye furaha ya asili na kuwa si wepesi kuwa na huzuni au kufadhaika.
 
Kazi hii ya mafuta ya habbat soda ndiyo mhimu kuliko zote sababu mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la kuwa na huzuni au stress na mifadhaiko ya akili kitendo ambacho kinaweza kuharibu kinga zao za mwili na maisha kwa ujumla.

Ni vigumu sana kupata mtishamba ambao unaweza kutibu matatizo yanayohusiana na saikolojia moja kwa moja lakini mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika kwa dhumuni hili la kutuliza, kupunguza na kutibu tatizo la huzuni au kufadhaika kwa akili.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
 
13. Chai ya Kijani

Watu wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo mara nyingi wanapungukiwa na nguvu na ujasiri. Na chai ya kijani inaweza kukurejeshea vyote hivi viwili yaani nguvu pamoja na ujasiri sababu ina kiinilishe mhimu kwa ajili kijulikanacho kama ‘L- Theanine’ ambacho hufanya kazi hii ya kuondoa mfadhaiko wa akili.

Hivyo kupunguza na kuondoa stress hakikisha hukosi kunywa chai hii mara 2 hata 3 kwa siku.
 
14. Chumvi

Unaweza ukashangaa kuona chumvi nayo imo kwenye orodha hii. Ukweli ni kuwa watu wengi hawatumii chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyao miaka ya sasa jambo linalopelekea wengi wao kupatwa na mfadhaiko wa akili na hata magonjwa kama shinikizo la juu la damu na kisukari.

Huwezi kuwa na afya bora kama hutumii ya kutosha kwenye vyakula vyako kila siku. Chumvi ni mhimu mwilini kama ilivyo kwa maji ya kunywa.
 
Chumvi ninayoizungumzia hapa ni ile yam awe ya baharini ambayo haijapita kiwandani kwakuwa ndiyo huwa madini madogo madogo (trace minerals) mhimu zaidi kwa afya ya binadamu.

Najuwa umeambiwa chumvi ni mbaya na kuwa unatakiwa ule vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, hata hivyo madai haya hayana ukweli wowote na ndiyo sababu unaona hata kwenye dripu la maji lazima na chumvi iwekwe ndani yake. Kila lita moja la dripu la maji ndani yake huwekwa chumvi gramu 9.
 
Chumvi inaweza kuwa mbaya ikiwa tu wewe si mtu unayependa kunywa maji mengi kila siku, ila kama unakunywa maji mengi kila siku basi unahitaji pia chumvi ya kutosha kwenye vyakula unavyokula kila siku.

Kama una msongo wa mawazo na unakula vyakula vyenye chumvi kwa mbali ni wakati sasa wa kubadili mtindo huo na hutakawia kuona mabadiliko mazuri.
 
15. LIMAU

Limau ni dawa nyingine ya asili rahisi ya kutibu msongo wa mawazo unayoweza kuiendea isiyo na madhara yoyote mabaya hapo baadaye kwenye afya ya mwili wako.

Ndiyo maana kila ukipewa supu asubuhi hawaachi kukuwekea na limau pembeni, kwakuwa limau huondoa uchovu na kujisikia vibaya kirahisi zaidi.
 
Tumia limau mara kwa mara kwenye kachumbali zako au unaweza kuchanganya vijiko vikubwa viwili vya maji ya limau ndani ya kikombe kimoja cha maji ya kawaida na unywe kila siku kutwa mara 1.

Usizidishe matumizi ya limau hata hivyo kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kupungua kwa kiasi cha damu mwilini mwako.
 
16. KABEJI

Imethibitika pasipo na shaka kuwa kabeji ni chakula bora kabisa ambacho kinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya aina mbalimbali za kansa, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, maambukizi mbalimbali, na mhimu kuliko yote ni kuwa kabeji inao uwezo pia wa kuzuia usipatwe na hamaki na mfadhaiko wa akili.
 
Kabeji lina vitamini B6, vitamini K na vitamini C. Ukiacha hayo kabeji pia ni chanzo kizuri cha folate, vitamini B1, potasiamu, copper, nyuzinyuzi (fiber) na manganizi. Viinilishe hivi ni mhimu sana katika kuichangamsha afya ya akili na mwili kwa ujumla.

Unaweza kutengeneza supu ya kabeji, juisi ya kabeji, kachumbali yenye kabeji ndani yake au ule tu mboga ya kabeji kila mara ili kupunguza stress yako bila gharama wala kutumia dawa yoyote yenye kemikali.
 
17. MAZOEZI YA VIUNGO

Mazoezi ya viungo ni dawa nyingine inayoweza kukuondoela msongo wa mawazo kirahisi zaidi bila gharama yoyote wala madhara yoyote katika afya yako.

Kuna watu mi nawaita kina chauvivu, kina chauvivu utawasikia ‘nakosa muda wa mazoezi’. Unakosa muda wa mazoezi mbona muda wa kulala hukosi? Huo ni uvivu tu ndiyo unakusumbuwa.
 
Back
Top Bottom