Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5. Jijengee mtazamo chanya ili kufanikiwa kwa viwango vikubwa.
Kama unafikiri huwezi kufanikisha ama kufikia kiwango fulani cha mafanikio katika maisha yako, basi hakuna njia nyingine ya kukutoa hapo, ndivyo itakavyokuwa. Kwa sababu kila hatua utakayochukua itaendana sawa sawa na kile unachoamini katika maisha yako siku zote.
 
6. Kila siku tafuta kubadilika kwanza wewe.
Ikiwa unataka maisha yako yabadilike. Anza kwanza kubadilika wewe. Hiyo ni njia rahisi ya kufikia mafanikio yoyote unayoyahitaji. Lakini ikiwa utakazana sana kubadili mambo ya nje na kujisahau wewe, itakuwa ni ngumu sana kwa wewe kuweza kubadilisha maisha yako zaidi utaendelea kubaki hivyo ulivyo.
 
8. Tafuta wazo moja na lifanyie kazi.
Najua unaweza ukawa unaweza mawazo mengi ambayo unataka kuyatendea kazi. Acha kuhagaika sana mara huku mara kule. Chagua wazo moja na kisha ulifanyie kazi. Ishi na wazo hilo na liwe kama sehemu ya maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…