Haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio, utafanikiwa.
Kiti kikubwa hapa, jifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha. Anayejizuia na kujikwamisha sio mwingine bali ni wewe mwenyewe na hali hasi nyingi ulizozibeba. Kuanzia leo amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa