Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mafuta mabaya (bad fat) 1.Saturated fat Ni aina ya mafuta ambayo mara nyingi yameganda ( solid at room temperature ) Matumizi ya aina hii ya mafita yanachangia kuongeza cholesterol kwy damu ambayo inachangia magonjwa ya moyo na kiharusi (stroke)hii ni kutokana na cholesterol ina jengwa kwenye kuta za damu na kufanya kuwa nyembamba, damu kiganda ambayo husababisha hayo magonjwa Vyakula vyenye saturated fat ni Nyama hasa nyekundu Mazao ya maziwa mfano jibini Siagi (butter) Mafuta ya kupikia yatokanayo na wanyama na nazi 2.trans fat Hii ni aina ya mafuta ambayo yanapatikana kwenye vyakula vilivyosindikwa /vyakula vya makopo, keki ,biskuti ,chips ambayo pia husababisha magonjwa ya moyo stroke Ni muhimu sana kujaribu kupunguza matumizi ya aina hii ya mafuta kwa afya bora
 
Karibuni kwenye afya bora tutaanza kuangalia aina mbalimbali ya mafuta ambayo ni mabaya kwa afya na mafuta ambayo ni mazuri kwa afya ya mwanadamu.Mafuta yamegawanyika katika sehemu kuu mbili 1.Mafuta mabaya (bad fat) ambayo yamegawanyika mara mbili saturated fat na trans fat 2.Mafuta mazuri (good fat )ambayo yamegawanyika mara mbili monounsaturated fat na polyunsaturated fat -
 
Mafuta mazuri (Good fats) 1.Monounsaturated fats Ni aina ya mafuta ambayo yanapatikana kwenye hali ya kimiminika na mara nyingi haya gandi na aina hii inasaidia sana kuondoa cholesterol mbaya na kupeleka kwenye figo ili kusaidia kusiwepo mafuta mengikwenye kuta za damu.Aina hii ya mafuta inapatikana sana kwenye mazao ya mimea Alizeti ambayo hutoa mafuta ya alizeti Mafuta ya mizaituni, parachichi,karanga ,korosho na mbengu mbali mbali 2.polyunsaturated fat Hii ni ya muhimu sana ambayo inatupatia omega 3 na omega 6 ambayo ni muhimu sana kwa afya. Vyakula vinavyotupatia omega 3 ni samaki hasa salmon, tuna ambao wana patikana baharini, kwenye karanga na mbogamboga za majani za kijani na pia kwenye maziwa ya wamama wanaonyonyesha Omega 6 inapatikana kwenye mafuta yatokanayo na mimea kama mafuta ya alzeti mafuta ya karanga. Ni muhimu sana kwa wamama wajawazito na wanaonyonyesha kwa ajili ya ukuwaji wa watoto So kula samaki japo mara moja kwa wiki Hivyo tujitahidi kula vyakula vyenye aina hii ya mafuta maana ni muhimu kwa afya ya binadamu na kujitahidi kupunguza vyakula vyenye mafuta mabaya -
 
Yogurt cup cake Mahitaji Unga wa ngano vikombe 3 Siagi kikombe 1 na nusu Maziwa mgando kikombe 1 na nusu Sukari kikombe 1 na nusu Vannila essence vijiko 2 vya chai Mayai 4 Baking powder 2 kijiko cha chai Baking soda nusu kijiko cha chai Njia Saga sukari na siagi mpaka iwe laini km dakika 10 kisha anza kuweka yai moja baada ya jingine kunaendelea kusaga mpk vichanganyike vizuri na kisha weka vannila kisha weka unga wako uliochekecha na kichanganya na baking powder na baking soda weka nusu unga kisha maziwa nusu koroga kisha malizia unga na maziwa yaliobaki koroga Chukuwa baking tin yako paka mafuta na kisha weka mchanganyiko wako Bake dk 30 kwy oven 200°c. Tayari kwa kuliwa -
 
Mazoezi ya kupunguza tumbo THE BICYCLE EXERCISE Lala chali huku mikono yako ikiwa chini ya kichwa chako, leta magoti yako kifuani huku ukinyanyua mabega juu. Taratibu leta kiwiko chako cha kulia hadi kwenye goti la kushoto huku ukinyoosha mguu wako wa kulia. Badili na upande mwingine na ufanye kama unakanyaga pedeli za baiskeli. Fanya zoezi hili seti 1-3 kwa kurudia mara 12-16.
 
Karanga husaidia kupunguza kansa ya utumbo Matumizi ya karanga ambayo ndani yana viturubisho folic acid, phytosterol, phytic acid and resveratrol ambayo husaidia kupambana na kansa ya utumbo Kula karanga mara 2 kwa wiki inasaidia kupunguza 27% ya kupata kansa kwa wanaume na marambili ya asilimia hiyo kwa wanawake
 
CARROT CAKE Mahitaji 2 1/2 kikombe cha karoti zilizosagwa 2 vikombe vya unga wa ngano 1 1/2 tsp baking powder 1 tsp baking soda 1 1/2 tsp mdalasini 1 1/2 kikombe cha sukari 1 kikombe cha mafuta ya kupikia 1 tsp vannilla essence 3 mayai Njia Chekecha unga wa ngano uliochanganywa na baking soda, baking powder na mdalasani. Chukuwa mayai anza kupiga kwa kutumia mashine km dakika moja kisha weka sukari na endelea kusaga mpk iwe nyeupe . Kisha weka mafuta na endelea kuchanganya na weka vannilla endelea kusaga. Kisha weka unga wako kwenye mchanganyiko na changanya vizuri kisha weka karoti na endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri. Bake kwa dk 45 mpk 60 na cheki kama imeiva kwa kutoboa katika na toothpick ikitoka safi tayari. Acha ipoe tayari kwa kuliwa ukipenda unapamba
 
CHOCOLATE BANANA CAKE Mahitaji 2 vikombe vya sukari 1 3/4 kikombe cha unga wa ngano 3/4 kikombe cha unga wa cocoa 1 1/2 tsp baking powder 1 1/2 tsp baking soda 2 mayai 1 kikombe cha ndizi zilizoiva zilizopondwa 1/2 kikombe cha maziwa 1/2 kikombe cha mafuta ya kupikia 1 1/2 vannila extract 1/2 tsp chumvi Njia Changanya unga wa ngano,sukari, baking powder, baking soda,unga wa cocoa na chumvi pamoja. Kwenye chombo kingine changanya mayai, ndizi zilizopondwa, maziwa ,vannila na mafuta ya kupikia mpaka ichanganyike vizuri. Kisha chukuwa huo mchanganyiko wa majimaji changanya na ule wenye unga changanya mpaka uchanganyike vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzito. Bake kwa dakika 40 mpk 60 na kisha angalia kama tayari kwa kuchoma na toothpick katika ikitoka safi tayari . Acha ipoe na tayari kwa kuliwa au kupambwa na chocolate , icing sugar na whipping cream.
 
Vitu tunavyotakiwa kula ili kutusaidia kuondoa sumu mwili (body detox) Maji husaidia sana kusafisha tumbo na kuondoa mafuta mwili. Tikitiki maji , matango na machungwa huondoa sumu na kuimarisha kinga ya mwili hasa inasaidia sana kuzuia kansa. Tangawizi, mdalasini na limao kwy chai husaidia kushafisha na kupunguza mafuta mwilini. Kula mboga za majani na kitunguu saumu husaidia sana kuondoa sumu mwili na kuongeza kinga ya mwili. Ni muhimu sana kuepuka vyakula vya makopo na juisi za viwandani ambayo ndizo kwa kiasi kikubwa vinachangia kuingiza sumu mwilini na kufanya mazoezi ni muhimu hasa husaidia kutoa sumu kupitia jasho. -
 
PISHI LA KEKI YA NAZI AU BASBUSA: MAHITAJI SUKARI CLASS 1 Unga wa samoule au wa sembe glass 1 Nazi ya machicha class 1 Unga wa ngano glass 1 Mafuta ya kupikia glass 1 Mayai 4 makubwa au yapime mayai yako sawa na kipimo cha glass Sukari vanilla kijiko cha chai 1 Baking powder kijiko cha chai 1 Mtindi kiasi vijiko 3 vyakulia MATAYARISHO Anza kupiga mayai pamoja na sukari na sukari vanilla kwa mda wa dakika 5 hadi 10 Kisha tia mtindi changanya vizuri Tia mafuta Changanya kisha mimina baking powder na unga unachanganya Kisha unatia unga wa samuole mwisho unatia nazi yako hakikisha unasaga had mchanganyiko wako uchanganyike vizur Andaa tray yako paka mafuta kisha tia unga ili keki yako isigande Mimina kwny trey washa jiko lako moto kiasi Koka keki yako had uone rangi unayoipenda na hakikisha ndani imeiva vizuri Ukiona tayar itoe anza kuikata vipande kiasi upendacho Huku ukiwa umeshaandaa shira yako mapema Kwa wasiojua shira unapika sukari vikombe 2 maji kikombe 1 na limau moja unaipika hadi iwe kiasi Kike yko ukiitoa kwny oven mimimia shira pale pale kabla ya kupoa KIDOKEZO ikiwa keki imoto basi shira iwe baridi au km shira imoto keki iwe baridi enjoys wnaopenda kufaham juu nimesaga lozi nimechanganya na nazi nikawekea juu ili kuleta muonekano nzuri
 
JINSI YA KUPIKA UBUYU : Sukari vikombe 2 Maji vikombe 2 Nusu kikombe unga wa ubuyu Vikombe 4 ubuyu wenyewe 1/4 pili pili ya unga 1/4 tsp chumvi 1/4 tsp iliki ya unga Rangi nyekundu au yeyote ile utakavyopenda. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate San kiasi tu. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe. Ukishapoa ubuyu tayari kuliwa. Enjoy
 
MAPISHI YA SWEET KWA KUTUMIA NAZI CHICHA MAHITAJI: Nazi chicha vikombe viwili Maziwa mazito kikopo kimoja Tunahitaji lozi kiasi Nazi chicha kidgo wa kupakia juu MATAYARISHI: changanya nazi pamoja na maziwa hakikisha unashikana katika hali ya kukata vidonge Kisha kata viduwara kiasi unachopenda Katika viduara vyako peleka kidole kwa ndani tia lozi moja moja kila kiduara Ukimaliza tumbikiza viduara vyako kimoja kimoja katika ile nazi kavu km unavoona ktk picha hapo itakua upishi wako upo tayar KITOKEZO: Unaweza kaweka ktka friji kama dakika 15 kisha unaweka nje unakula mda unaopenda au cku unayopenda usipopenda kutia ktk friji pia haileti madhara Enjoy
 
Back
Top Bottom