Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utakapochemsha, utauwa wadudu wanaodhuru, na wale wasioudhuru wamejaa
tele hewani, maziwa yote yataganda bila wasiwasi. Tujihadhari sana na
maziwa ya mgando ya mitaani, mabarabarani na hata migahawani. Wengi
wao hawachemshi kabla ya kugandisha. Iwapo utakuwa na hamu sana,
jiandalie kwako. Nunua fresh, chemsha, gandisha kwa ajili ya kesho.
Takriban masaa manane hadi kumi maziwa yaliyochemshwa huanza kuganda.
Hivyo waweza kuchemsha jioni na kutumika asubuhi au kuyagandisha
asubuhi na kunywewa jioni.
 
Maziwa ya maji ya kwenye makopo au vifuko vya karatasi au nailoni ni
aina nyingine ya maziwa. Tunaiita hii kuwa ni aina nyingine ya maziwa
kwa sababu kadhaa, mojawapo ikiwa ni kule kupitia kiwandani. Maziwa
halisi hupelekwa viwandani na kufanyiwa mabadiliko kadhaa.
 
Wakati mwingine huongezwa virutubisho na hata kuchanganywa na sukari
nyingi. Yale yenye sukari nyingi hudumu zaidi hata yanapofunguliwa
kwani sukari huzuia wadudu kukua. Mara nyingi maziwa haya virutubisho
vyake huharibiwa na madawa wakati wa utayarishaji. Pamoja na kuwa huwa
wanaongeza virutubisho vingine, si mara zote huwa wanakuwa sahihi.
 
Jitahidi kila iwezekanavyo kunywa maziwa halisi kuliko yanayopitia
viwandani. Ni jambo muhimu kuzingatia tarehe ya mwisho ya kutumika
maziwa hayo. Ni lazima iandikwe kwenye kopo au kijifuko cha
kuhifadhia. Ni jukumu la serikali kupitia shirika lake la viwango
(TBS) kuhakikisha tarehe hizo ni za kweli au za kibiashara zinapelekea
wanywaji (watumiaji) kuathiri afya yao. Kwa upande mwingine ni jukumu
la mtu binafsi kuwa makini na kila anachokula kinywani.
 
Aina ya mwisho ya maziwa ni maziwa ya unga (died milk). Maziwa halisi
huondolewa maji yote na kubakia unga. Vitamini zote ambazo huwepo
katika maji hupotea, kama vitamini C na B. Lakini virutubisho vingine
hubakia. Lakini yapo maziwa mengine huondolewa maji pamoja na mafuta.
Haya huitwa (died skimmed milk)
 
Maziwa haya virutubisho hivyo kwa njia nyingine. Ni vizuri sana
kuchunguza makopo au mifuko iliyohifadhiwa maziwa haya kuona ni ya
aina gani na viwango vya virutubisho vilivyowekwa. Usipoteze pesa zako
kwa kununua kitu kibovu. Maziwa yaliyo mazuri ni yale yaitwayo "whole
died milk" ambayo yameondolewa maji tu. Kwa sehemu ambazo maziwa
halisi ni vigumu kuyapata au hupatikana katika mazingira machafu, ni
bora familia kutumia maziwa ya unga. Lakini kumbuka kuangalia tarehe
ya kuharibika kila kilichopitishwa tarehe yake ya kutumika ni sumu.
 
Kwa upande mwingine, kuna maziwa ya unga ambayo hutengenezwa kwa ajili
ya watoto. Haya huchanganywa na virutubisho mbalimbali ili kujaribu
kuyalinganisha na maziwa ya mama. Hakika hilo haliwezekani kamwe.
Iwapo mwanao itabidi atumie maziwa ya unga, angalia usije ukamnunulia
maziwa ya wakubwa.
 
Back
Top Bottom