Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_3504.PNG
 
MADEREVA KAMA MNATAKA KUJIUA MSITUSHIRIKISHE
Nimewaza sana kuhusu madereva wa bongo, yaani kila nikiwaza najikuta jibu ni moja tu, madereva wa siku hizi ni tofauti sana na enzi zetu. Enzi zetu barabara zilikuwa nyembamba, magari machache tena sio mazuri kama siku hizi, ilikuwa kawaida sana kusikia ajali imetokea kwa kuwa steringi imekatika, au tairi limechomoka, mara nyingine utasikia breki zimefeli
 
Lakini siku hizi magari yameboreshwa, si rahisi kusikia eti steringi ilichomoka au breki zimefeli lakini ajali ndio zimeongezeka sana. Enzi zetu pikipiki pia zilikuwa za kizamani hazina indiketa, pikipiki zilikuwa na breki za waya ambazo uliweza kusikia zimekatika wakati wowote. Pamoja na hali hiyo ajali za kizembe zilikuwa chache sana.
Sasa siku hizi kama nilivyosema gari zimeboreshwa, pikipiki zimeboreshwa, barabara zimeboreshwa sasa eti madereva nao wameboresha ajali.
 
Madereva wa bodaboda wakiona ajali haziwatokei huamua kuvuka taa nyekundu bila kuangalia kushoto wala kulia. Madereva wa magari nao wakiona siku nyingi hawajapata ajali wanaanza kutuma meseji wakati wanaendesha gari. Sio ajabu ukasikia dreva wa basi aliovateki kwenye kona akiwa spidi kali. Sasa naomba nitoe ushauri kwa serikali. Nimefanya utafiti wa siri nyumbani kwangu, nimegundua kuwa kuna madreva wanakuwa wana ajenda ya siri wawapo barabani. Yaani jama unamuona freshi kabisa anaongea na wewe anacheka kumbe ndani anampango wa kujiua.
 
. Au siku hiyo ana hamu ya kuuwa mtu. Dreva akitaka kujiua utaona anachukua simu na kuanza kuchati kwenye simu huku anaendeesha, hapo ujue anatafuta taimingi abamizwe afe. Kama ni dreva wa bodaboda au bajaji, utamuona anajipitisha katikati ya magari kwa spidi moyoni anaomba abamizwe afe. Sasa kuna ule wakati dereva anakuwa na hamu ya kuuwa mtu, hapo ndipo ataanza vituko hivyohivyo huku akiwa na abiria, hapo anajua akikosa kumuua abiria basi atampata mtembeea kwa miguu. Sasa baada ya utafiti huu, nashauri trafiki mkimkamata dreva anavunja sheria barabarani sio mnamtwanga faini, haisaidii, mchukueni kwanza mkampime mkojo kama kavuta bangi, kisha mpelekeni kitengo cha kupima akili, ndipo ijulikane adhabu stahiki
 
HAYA KACHUKUE SIMU YAKO SUPAMAKETI
BINTI mmoja alisahau simu yake supamaket. Meneja wa supa maketi aliangalia kwenye phone book na kukuta namba imeandikwa 'Mama'. Akapiaga na mama akapokea;
MENEJA: Shkamoo mama mwanao kwa bahati mbaya amesahau simu yake hapa supamaket, unaweza kumtaarifu aje aichukue?
MAMA: Marahaba mwanangu, hakuna tabu na asante sana, nitamtaarifu sasa hivi.
Baada ya sekunde chache simu ikaanza kuita, jina lililotokea ni 'Mama', meneja akapokea na kabla hajajibu mama akaanza kuonea
MAMA: We Fulo, angalia ujinga wako sasa, simu umeenda kuiacha supamaketi, haya nenda ukaichukue sasa hivi usirudi bila simu.
 
YANAYOENDELEA KWENYE SUPAMAKETI NI VITUKO PLUS
Juzi niliamua kuzunguka mjini kuangalia vituko vya maendeleo. Yaani we acha tu, ushishangae kuona fenesi zimefungwa kwenye glasi za juis, wala usishangae kuona chandarua kimegeuzwa neti ya kuvulia samaki, mambo yako shaghala baghala.
Lakini shaghala baghala kubwa niliikuta nilipoingia supa maketi.
 
Baada ya kuchunguza kwa makini nikagundua kuna kitu cha ajabu sana kinaendelea ndani ya supamaketi zetu, kumbe sio kila anaeingia supamaketi anaingia kununua bidhaa, watu wana sababu mbalimbali. Aina ya kwanza ya wateja ni wale wanaoingia kujipiga picha, wenyewe wanaziita selfie, yaani hawa wako kibao kila kona unakuta mtu anajipiga picha
 
Back
Top Bottom