uliingia supamaket. Hawa huishia kununua mkate, au chumvi, wakijitahidi wataongeza na blubendi. Halafu kuna kundi la wamama washua, hawa huingia supamaketi na kikaratasi kimeandikwa kila kitu wanachotaka kununua, bahili hao, utakuta wanatembea na kalkuleta, wanaenda hesabu sambamba na mhudumu, mara nyingi hawa huja na watoto wao wakorofi, wanakimbia kimbia hovyo supamaketi, na ni wazi wanasoma intanesho, maana utasikia wamama hao kila dakika wakiita ‘ Junia, junia kam hia, Juni no stop that’ Wazungu weusi flani hivi.