Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ndugu yangu nakwambia watu wenye mapengo ni watu wa levo nyingine kabisa. Ukimuona mtu ana mapengo mpe shikamoo. Mtu mwenye mapengo ni mtu shujaa, usijilinganishe nae kabisa. Wiki iliyopita niliamka fresh kama kawaida, nikatimka home na kwenda kwenye mishemishe mbalimbali. Mida ya saa sitasita kama kawa tumbo likaanza kudai mshahara wake, nikaingia kwa mama ntilie mmoja nikaagiza wali maharage na kikombe cha chai,
 
, mi napenda sana chai, hata saa sita ya mchana jua la Jiji la Dar halinishawishi kuacha kusindikiza wali maharage kwa chai, au hata chips mayai kwa chai kwangu safi tu. Basi nikaanza kuutendea haki wali ule. Nadhani kilikuwa kijiko cha saba au cha tisa nikiwa katika furaha kubwa si nikatafuna bonge ya jiwe kwenye wali? Tena nikatafunia jino ambalo lilishawahi kuanza kuuma uma kidogo, ndugu yangu hayo maumivu niliyoyasikia yalinifanya nisahau niko wapi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…