Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

chozi likanidondoka bila kupenda mwanaume. Nikainama naugulia nangojea maumivu yapungue,wapii. Niliinuka na kuanza kuondoka bila kulipa, na mama ntilie mwenyewe hakutaka hata kunidai alijua kuwa hilo kosa lake. Siku ikawa ndo imeharibika, nikapanda basi niikarudi home. Nikatafuta panado nikameza nikajilaza haikusaidia kitu, mama mmoja mpangaji mwenzangu mmbeya mmbeya akanambia ana mafuta ya karafuu nipake kwenye jino, nikapaka nikajilaza masaa yakapita jino halitaki kupoa
 
Giza likaanza kuingia mzee mzima machozi yalikuwa yanatoka bila aibu. Jirani yangu chumba cha pili ndio akatoa shauri nikang’oe. Sikubisha maana maumivu yalikuwa balaa, japo kichwani nilikuwa naogopa sana ishu ya kung’oa jino, lakini kwa maumivu niliyokuwa nayapata, nilikuwa tayari kwa chochote. Jirani akanisindikiza mpaka hospitalini, kufika kule tunaambiwa daktari wa meno hayupo mpaka kesho yake asubuhi. Tukageuza kurudi home kichwani nawaza ntawezaje kufika
 
mpaka kesho yake asubuhi na maumivu makali yale? Ulikuwa usiku mrefu sana, akilini nilikuwa nawaza kuwa asubuhi mapema nawahi kung’oa jino. Alfajiri kama saa kumi na moja hivi nikapitiwa na usingizi, nikashtuka saa mbili na nusu. Jino limetulia, linauma kwa mbali. Nikaanza kuona kuwa kung’oa sio muhimu kiviiile. Jirani akang’ang’ania ning’oe utadhani jino lake, ‘Ohh kang’oe bwana hilo jino litaanza
 
kuuma tena’ na maneno mengine ya aina ile kupunguza kero nikakubali ntaenda hospitali. Basi kweli nikaenda hospitali nikaandikisha kila kitu na kukaa kwenye foleni ya kusubiri kumuona daktari wa meno. Ndugu yangu foleni ile inatisha, mtu mmoja mmoja anaingia kwa dokta, halafu unasikia kilio humo ndani,'Aaaaaaaah', mwanaume mzima analia, kisha akitoka anatoka kwa hatua ndefu utadhani ana safari ya kwenda mji mwingine kwa miguu, kanuna, jasho linamtoka, aisee inatisha.
 
Nikawa taratibu nasogea kadri watu walipokuwa wanapungua, hofu nayo ilinizidi. Kiukweli nilishindwa kuvumilia nilipoona nimefikia kuwa mtu wa tatu, niliulizia choo cha wanaume kiko wapi, nilipotoka hapo sikugeuka nyuma mpaka nilipofika home. Jino bado linanikong’ota kila siku tena siku hizi linaanza kuuma saa sita mpaka saba usiku, lakini kung’oa naogopa. Ndio najiuliza hivi hawa wenye mapengo wanaokubali kung’olewa hata meno manne ni mashujaa kiasi gani? Shkamoo wenye mapengo
 
Back
Top Bottom