lilichomwa moto na wakazi wa kijiji cha Mwakaleli kwasababu lilikuwa likileta mikosi mingi kijijini hapo ikiwemo vifo vya mara kwa mara kitu ambacho si sahihi kitaalam ziwa haliwezi kuhama, Zipo imani miongoni mwa watu kuwa ziwa ngosi watu wanapotea kimazingara, kuwapo kwa sauti za watu wasioonekana ndani ya misitu, wengine husema ziwa hilo limekuwa likigeuka rangi mara kwa mara na kuwa na rangi za kijani, bluu, nyeusi na nyeupe kitu ambacho kinawafanya waamini kuwa ziwa hilo sio la kawaida.