Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika safari yetu ilitubidi kugawa makundi mawili ya watu 15 ili kurahisisha kutambuana ambapo kundi namba moja (1) lilikuwa chini ya modesto winfred na kundi namba mbili(2) lilikuwa chini ya amos asajile, hivyo washiriki wote tulifika kituo cha kwanza mnamo saa 4:30 Na kupumzika kwa muda wa dakika 20, ndipo tulipoanza safari kueleke kituo cha pili ambapo ilikuwa ndio sehemu ya juu ya milima inayolizunguka ziwa ngosi tulipumzika na kupata chakula cha mchana, mahali hapa palikuwa na upepo mwanana na baridi kali sana iliyopelekea watu wote kuvaa tena masweta yetu.
 
Hatukuishia hapo ndipo safari ikaanza tena na hapa ndipo kindumbwe ndumbwe kikaanza kwani ilikuwa sehemu ngumu sana ambayo ikapelekea idadi kubwa ya watu kushuka kwa kutumia makalio, baada ya kumaliza kile kilima ndipo moja kwa moja tukaingia katika ule msitu mnene mithili ya Amazon kutokana na kukosekana kwa alama zenye kuonyesha muelekeo kundi namba mbili (2) tukapotea na kujikuta tukielekea usawa wa afrika kusini badara ya kwenda ule upande viliko visiwa.
 
Hatukuishia hapo ndipo safari ikaanza tena na hapa ndipo kindumbwe ndumbwe kikaanza kwani ilikuwa sehemu ngumu sana ambayo ikapelekea idadi kubwa ya watu kushuka kwa kutumia makalio, baada ya kumaliza kile kilima ndipo moja kwa moja tukaingia katika ule msitu mnene mithili ya Amazon kutokana na kukosekana kwa alama zenye kuonyesha muelekeo kundi namba mbili (2) tukapotea na kujikuta tukielekea usawa wa afrika kusini badara ya kwenda ule upande viliko visiwa.
 
Na kibaya zaidi ni kwamba Muwapo ndani ya msitu huo hakuna simu inayoshika kutokana na kukosekana kwa mtandao hivyo ikawa ngumu kuwasiliana na kundi namba (1) lakini tulipofika mbele tukakuta njia haionyeshi kuwa kuna watu wamepita hivyo tukarudi nyuma na kuikuta njia ambayo wenzetu walipita hivyo kundi namba moja waliwahi kufika lakini kundi namba mbili tukachelewa kidogo kufika.
 
Kutokana na maelezo tuliyokuwa tumepewa na Tanzania forest services nyanda za juu kusini ilikuwa ngumu kuwaruhusu watu kuogelea hivyo hakuna mdau yeyote aliyeogelea ziwani hapo kwa sababu za kiusalama. Tukapumzika kidogo na kisha tukaanza ratiba ya michezo na matukio mbali mbali kama yalivyokuwa yameandaliwa kama vile kutaja vivutio vipatikanavyo maeneo ya mkoa wa Mbeya (Naijua Mbeya Kuliko wewe), kukimbia na yai katika kijiko na shindano la hisia (kulia) ambapo washindi waliopatikana walikabidhiwa zawadi zao kutoka kwa taasisi wadhamini wa mashindano hayo, mara baada ya kumaliza hayo ndipo saa 9 jioni tukaanza safari ya kurudi kwa makundi kama awali.
 
Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu aliyekuwa pamoja nasi katika safari yetu kwani wote tulikwenda salama na kurudi salama hakuna hata aliyeumia katika safari hii. Pia tupende kutoa shukrani zetu za dhati kwa taasisi wasiriki, kamati ya utalii ya mkoa wa mbeya na wadau wote walioshiriki ambao kiukweli kutokana na wingi wao itakuwa ngumu kuwataja kwa majina.
 
Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinakwamisha sana kukua ama kufahamika kwa ziwa ngosi miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na, Miundo mbinu mibovu ambayo hupelekea watalii kushindwa kufika kwa urahisi katika eneo husika, Viongozi wachache wa safari (tour guides), Matangazo ya kivutio, Taarifa na maelezo hafifu ya kivutio, Makosa ya matamshi ya jina.
 
Pamoja na hayo Jitihada muhimu zinahitajika ikiwemo kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababisha udongo kuingia ziwani hivyo kupunguza kina cha ziwa, kujenga angalau ngazi zenye sehemu za kujishikiria katika baadhi ya maeneo ambayo ni tatanishi/magumu kupanda ama kushuka, vyombo mbali mbali vya habari kujitokeza kwa wingi kulitangaza ziwa ngosi, pia kujenga kijisehemu kidogo ambacho kitatoa huduma muhimu ikiwemo chakula na vinywaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…