Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KULALA
Kwa wastani mtu mzima katika hali ya kawaida anatakiwa alale kwa muda wa saa 6 hadi 8.Unapolala Usingizi ndio wakati ubongo unafanyakazi yake vizuri ya kuhifadhi kumbukumbu.Epuka kulala mara tu baada ya kula chakula.Ni vizuri unapolala kulalia ubavu wa kulia au chali.Hakikisha unalala sehemu safi.Uwe na nguo maalum ya kulalia zisizozakubana.Ni vizuri kusafisha mwili(kuoga) na kinywa(kupiga mswaki) kabla ya kulala.
 
HUU NDIYO WASTANI WA KIWANGO CHA KUPATA USINGIZI
Ni kama ifuatavyo:
Umri wa miaka 2 anatakiwa kulala saa 14 hadi 16 kwa siku.
Umri wa miaka 4 saa 12 hadi 14 kwa siku.
Umri wa miaka 6 hadi 11 saa 10 hadi 11 kwa siku.
Umri wa miaka 14 hadi 18 saa 8 hadi 9 kwa siku.
Watu wazima wanahitaji saa 6 hadi 8 za kulala.
Hizi ni baadhi tu ya njia za kuzuia au kupunguza Msongo wa Mawazo na Mfadhaiko.
 
Mabaraza ya jiji hujaribu kusafisha barabara kwa kuzoa takataka, hata hivyo, takataka hurundamana katika sehemu fulani ambako hazivutii na kuwa tisho kwa afya ya umma. Takataka zinaporundamana zinaweza kuongeza idadi ya panya, mende, na viumbe wengine wanaoweza kusababisha magonjwa. Je, kuna lolote unaloweza kufanya kuhusu jambo hilo? Bila shaka, hakikisha kwamba nyumba na mazingira yako ni safi na nadhifu.
 
Mtazamo wa Akili Unaofaa

Watu wengine hufikiri kwamba watu maskini hawawezi kuishi katika nyumba na mazingira safi. Hata hivyo, si lazima iwe hivyo. Kwa kweli, kukosa pesa kunaweza kufanya iwe vigumu kudumisha mazingira yetu yakiwa safi. Lakini methali moja ya Kihispania inasema, “umaskini na usafi hazipingani.” Kwa upande mwingine, kuwa na pesa hakumaanishi kwamba mtu atadumisha mazingira yake yakiwa safi.
 
Mtazamo wa Akili Unaofaa

Watu wengine hufikiri kwamba watu maskini hawawezi kuishi katika nyumba na mazingira safi. Hata hivyo, si lazima iwe hivyo. Kwa kweli, kukosa pesa kunaweza kufanya iwe vigumu kudumisha mazingira yetu yakiwa safi. Lakini methali moja ya Kihispania inasema, “umaskini na usafi hazipingani.” Kwa upande mwingine, kuwa na pesa hakumaanishi kwamba mtu atadumisha mazingira yake yakiwa safi.
 
Kudumisha usafi ndani na nje ya nyumba hutegemea mtazamo wa akili ambao humchochea mtu atende. Kwa kweli, kudumisha nyumba ikiwa safi hutegemea mtazamo wa akili wa familia yote. Kwa sababu hiyo, inafaa tuchunguze yale tunayoweza kufanya ili kuchangia usafi wa nyumba zetu, kutia ndani ujirani wetu.
 
Ratiba ya Usafi

Inaonekana kwamba kazi ya akina mama haiishi. Licha ya kupika na kuwatayarisha watoto kwa ajili ya shule, lazima wasafishe nyumba ndani na nje. Je, umeona kwamba mara nyingi mama ndio huokota nguo chafu au vitu vingine ambavyo watoto huacha katika vyumba vyao? Ratiba nzuri ya usafi inayohusisha kila mtu katika familia inaweza kumpunguzia mama kazi.
 
Ratiba ya Usafi

Inaonekana kwamba kazi ya akina mama haiishi. Licha ya kupika na kuwatayarisha watoto kwa ajili ya shule, lazima wasafishe nyumba ndani na nje. Je, umeona kwamba mara nyingi mama ndio huokota nguo chafu au vitu vingine ambavyo watoto huacha katika vyumba vyao? Ratiba nzuri ya usafi inayohusisha kila mtu katika familia inaweza kumpunguzia mama kazi.
 
Wake fulani huwa na ratiba ya kushughulikia na kusafisha vitu fulani kila siku, kusafisha sehemu fulani za nyumba mara moja kwa juma, na nyingine mara moja kwa mwezi. Hata kuna vitu vinavyoweza kuratibiwa visafishwe mara moja kwa mwaka. Kwa mfano, katika Makao ya Betheli, kwenye ofisi za tawi za Mashahidi wa Yehova katika kila nchi, sehemu za kuwekea nguo na kabati husafishwa mara moja kwa mwaka. Huo ni wakati wa kutupa vitu visivyotumiwa na kupanga kabati hizo. Pia kuna ratiba ya kawaida ya kusafisha kuta.
 
Ili kila mtu awe na afya nzuri, kuna sehemu fulani katika nyumba ambazo zinapaswa kudumishwa zikiwa safi, kama vile choo na bafu. Ingawa zinapaswa kusafishwa kidogo kila siku, sehemu hizo zinapaswa kusafishwa kabisa labda mara moja kwa juma ili kuzuia bakteria zisiongezeke. Wengine hufikiri kwamba madoa ambayo huwa katika bakuli la choo hayawezi kuondolewa. Lakini, kuna nyumba ambazo choo huwa safi kabisa na hung’aa. Unahitaji tu kusafisha kwa ukawaida na kutumia sabuni zinazofaa.
 
Jikoni pia kunahitaji kusafishwa vizuri. Ingawa kila siku mtu husafisha vyombo, jiko, na meza, mara kwa mara, labda mara moja kwa mwezi, ni muhimu kusafisha mahali ambapo jiko na vifaa vingine vya kupikia huwekwa. Kusafisha kabati na stoo kwa ukawaida kutazuia mende na wadudu wengine wanaoweza kudhuru wasifanyize makao humo.
 
Ushirikiano wa Familia

Wazazi fulani wamewawekea watoto wao sheria na kuwazoeza kwamba kila mara kabla ya kutoka katika vyumba vyao asubuhi ili kwenda shuleni, wanapaswa kutandika vitanda, kuweka nguo chafu mahali panapofaa, na kupanga vitu vyao vingine. Sheria inayofaa ni, “Kila kitu kina mahali pake na basi kila kitu kinapaswa kuwekwa mahali pake.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…