Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ushirikiano wa Familia

Wazazi fulani wamewawekea watoto wao sheria na kuwazoeza kwamba kila mara kabla ya kutoka katika vyumba vyao asubuhi ili kwenda shuleni, wanapaswa kutandika vitanda, kuweka nguo chafu mahali panapofaa, na kupanga vitu vyao vingine. Sheria inayofaa ni, “Kila kitu kina mahali pake na basi kila kitu kinapaswa kuwekwa mahali pake.”
 
Pia, watu fulani katika familia wanaweza kugawiwa kazi au eneo hususa liwe sehemu yao ya kusafisha. Kwa mfano, je, baba huhakikisha gereji imepangwa na kusafishwa kabisa angalau mara moja kwa mwaka? Je, mtoto mmoja anaweza kumsaidia? Nani huhakikisha kwamba hakuna magugu au nyasi ndefu mbele ya nyumba? Hilo linapaswa kufanywa mara ngapi ili kuhakikisha eneo la mbele la nyumba ni nadhifu? Je, nyumba ina dari au stoo inayohitaji kuondolewa vitu visivyohitajika na kupangwa vizuri? Ikiwa ndivyo, ni nani atafanya kazi hiyo? Wazazi wengine hugawia watoto kazi hizo, wakizibadili kwa zamu.
 
Kwa hiyo, panga ratiba nzuri ya kutunza nyumba yako. Iwe utasafisha nyumba mwenyewe au pamoja na familia yako au utahitaji kumwajiri mtu akusaidie, ni muhimu kuwa na ratiba nzuri. Mama mmoja ambaye hudumisha nyumba yake ikiwa safi sana anatueleza jinsi familia yote hushirikiana kuisafisha: “Mimi na binti zangu watatu hugawana kazi za nyumbani. Norma Adriana husafisha sebule, vyumba viwili vya kulala, ua, na eneo la mbele la nyumba. Ana Joaquina hushughulika na jikoni. Mimi huosha nguo na kushughulikia mambo mengine, naye María del Carmen huosha vyombo.”
 
Sura Nzuri Nje ya Nyumba

Namna gani nje ya nyumba? Iwe unaishi katika nyumba kubwa au katika nyumba ya hali ya chini, unahitaji kuwa na ratiba ya kusafisha na kudumisha usafi wa nje. Kwa mfano, lango katika ua wa nyumba linaweza kung’oka bawaba moja. Lango hilo litaonekana vibaya ikiwa halitarekebishwa. Pia kutaonekana vibaya ikiwa takataka zitaachwa zirundamane kwenye mwingilio wa nyumba au kwenye vijia vya karibu. Nyakati nyingine pia, mikebe na vitu vingine huachwa nje ya nyumba na vinaweza kuwa makao ya wanyama na wadudu waharibifu.
 
Familia fulani zimepanga kufagia na kusafisha sehemu za nje za nyumba, kutia ndani vijia vya kando na hata barabara mbele ya nyumba, mara moja kwa siku au kila juma inapohitajika. Ni kweli kwamba katika maeneo fulani serikali zina mipango mizuri ya kusafisha mazingira, lakini kwingine hakuna mipango kama hiyo. Bila shaka, mahali tunapoishi pataonekana safi zaidi na hapatakuwa hatari kwa afya ikiwa sote tutatimiza sehemu yetu kupasafisha.
 
Zaidi ya kupanga ratiba ya kazi zilizotajwa, familia fulani huandika ratiba yao na kuibandika mahali kila mmoja anaweza kuiona na kuifuata. Hilo linaweza kuwa na matokeo mazuri. Kwa kweli, hatujaorodhesha mambo yote unayopaswa kujua kuhusu usafi. Kwa mfano, unahitaji kuamua bidhaa za kusafishia zinazofaa eneo lenu na vifaa ambavyo unaweza kununua.
 
Bila shaka, mapendekezo haya machache yatasaidia familia yote ielewe uhitaji wa kudumisha usafi wa nyumba na mazingira yake. Kumbuka kwamba kudumisha nyumba na mazingira yake yakiwa safi kunategemea si kiasi cha pesa ulizo nazo, bali mtazamo wako wa akilini.
 
Ratiba Unayoweza Kutumia Kusafisha Nyumba

Tumia nafasi ya ziada kuongeza mambo yako mwenyewe kwenye orodha hii

Jambo muhimu: Kuchanganya bidhaa za kusafisha kunaweza kuwa hatari sana. Hasa jihadhari dhidi ya kuchanganya dawa ya kuondoa madoa na amonia
 
20968532_349747685482532_7227390143290671104_n.jpg
 
Back
Top Bottom