Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu wenye ngazi za chini ya kujithamini huwa wanaruhusu wengine kuwatendea vibaya, hawajijali, na wana ugumu kuwa peke yao. Zaidi ya hayo, wana hali ndogo ya kujiamini na kwa hiyo wanazuia kuthubutu na wanaamini kwa shida kama watu wengine wanawajali. Watu wenye kiwango kidogo cha kujiamini wanapenda kuchukulia vitu kibinafsi, muda mwingine wanaonekana kama ni rahisi kuchukuliwa na fikra kupita kiasi na mtu asiyeridhika na chochote mbali na anachofikiri kuwa ndicho, wanajikosoa wenyewe na
 
wengine, na huamini kwamba hawawezi kufanya chochote kwa usahihi. Watu hawa huwa wana tabia ya kuona kuwa mambo yote ni mabaya juu ya maisha, na wanajiona kana kwamba hawastahili kuwa na bahati nzuri.

Kujitegemea Kimawazo

Watu wenye kiwango kidogo cha kujithamini pia wana kiwango kidogo cha
 
kujitegemea kimawazo, kwa maana kwamba picha yao ya ndani, jinsi gani wanajiona, ni mbaya sana. Kwa sababu ya hiki kiwango kidogo cha kujitegemea kimawazo, watu wenye kiwango kidogo cha kujithamini wana hatari zaidi ya kuwaruhusu wengine kuwatendea vibaya au kuwatumia vibaya, na kushindwa kudai haki yao.
 
Matatizo mengi ya kisaikolojia na nguzo zao katika kiwango kidogo cha kujithamini, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kula, matatizo ya madawa ya kulevya, huzuni, na ugonjwa wa wasiwasi.

Tunapata wapi kujithamini kwetu? Watu wengi watasema wanapata kutoka kwa wazazi wao, waalimu, rika lao, ndugu,
 
taasisi za kidini, na vyombo vya habari. Wakati mambo haya kwa hakika yanaweza kuathiri kujithamini kwetu kwa uzuri au kwa ubaya, yote ni mambo ya nje. Kujithamini inashabihiana na mtazamo binafsi wetu wa ndani. Kama kujithamini kweli kunakuja kutoka mwonekano wetu wa nje, basi kuna haja ya kubadili mazingira yetu na watu wanaotuzunguka. Hii ndio sababu kwamba watu hupenda kujiambia, “Ikiwa
 
ningetengeneza hela zaidi, ningekuwa na gari zuri, ningekuwa nimeoa/nimeolewa, au ningekuwa na kazi ya kifahari, ningejisikia vizuri sana.” Hii inaweza kuwa mzunguko wa matatizo, kumuacha mtu muda wote akitafuta zaidi, na daima haridhiki. Hii pia inaweza kumsababishia mtu kuwa na hali ya kutoridhika na chochote mbali na anachofikiri kuwa ndicho na kutojikubali yeye mwenyewe.
 
Inakubalika kiujumla kwamba kujithamini huja kutoka ndani mwetu na hatimaye ndani ya udhibiti wa kila mtu. Zaidi ya hayo, kujithamini haimo kwa wote au hakuna ambaye hana kabisa, watu wengi wana viwango mbalimbali vya kujithamini, kutegemea juu ya hatua zao za maendeleo, matukio kwenye maisha yao, na mazingira yao.
 
Akili ya Kihisia

Kipengele cha tatu cha afya ya kisaikolojia ni kiwango cha akili ya kihisia ulichonacho. Akili ya hisia inahusu “uwezo wa kuwaelewa wengine na kutenda kwa busara kwenye mahusiano ya binadamu.” Zaidi ya hapo, akili ya kihisia inaweza kugawanywa katika nyanja kuu 5:
 
Kujihamasisha mwenyewe. Watu wanaoweza kujihamasisha wenyewe huwa na kuwa wazalishaji wa hali ya juu zaidi na wako huru kuliko wale wanaotegemea nguvu kutoka vyanzo vya nje kuwahamasisha. Jinsi unavyoweza kujihamasisha zaidi na kushiriki katika shughuli zenye malengo, ndivyo unavyozidi kuikuza akili ya kihisia yako.
 
Kujua hisia zako. Hii inachukuliwa kuwa ni msingi wa akili ya kihisia na inahusiana na kwa kiasi gani una hali ya kujitambua na ufahamu ulio nao. Una haraka kiasi gani kuweza kutambua na kuzipachika hisia zako kwa jinsi unavyozihisi kuamua kiwango chako cha akili ya kihisia.
 
Kusimamia hisia zako. Ni kwa uzuri kiasi gani unaweza kuonesha hisia zako ipasavyo na kukabiliana na hisia zako? watu wenye shida ya kukabiliana na wasiwasi, dhiki, na kushindwa huwa wana viwango vidogo vya akili ya kihisia.
 
Kutambua hisia kwa wengine. Kipengele kingine cha akili ya kihisia ni kiwango chako cha kutambua hisia za wengine ambacho unacho au ni mwepesi kiasi gani kuhisi hisia za wengine na jinsi gani unajumuika na watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…