Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Madhara yatokanayo na mzio
Dk Fazel anasema madhara ya mzio ni pamoja na kupata shambulio kali ambalo linaweza kusababisha kifo kama matibabu hayatafanywa haraka.
Kuna baadhi ya watu ambao wakila baadhi ya vyakula huvimba mwili na kushindwa kupumua mpaka kuhitaji kulazwa hospitali na kusaidiwa kupumua kwa mashine.
Madhara mengine ni pamoja na shida ya kuvuta pumzi au kushuka kwa shinikizo la damu (kupata shock).
 
Namna ya kujikinga na aleji
Dk Fazel anasema kuna baadhi ya wagonjwa hupata madhara makubwa ya kuungua nje na ndani pindi wanapotumia dawa ambazo zina sulfer na huwasababishia mzio ambao usipotibiwa kwa haraka, kifo kinaweza kutokea.
“Steven Johanson’s syndrome ni mzio hatari na wa kipeke kuliko aina zote na mgonjwa
 
anapopata aina hii ya mzio na ngozi yake huungua nje na ndani na endapo akichelewa kupewa matibabu huweza kupoteza maisha,” anasema Dk Fazel.
Jinsi mzio unavyonyima uhuru wa kufanya kazi
Evelyn Menas mkazi wa Mtoni Kijichi, anasema yeye mara nyingi hupata tatizo la mzio akikaa au kupita eneo lenye vumbi au kutokwa na jasho mwilini, mambo yanayomnyima uhuru wa kufanya kazi katika baadhi ya mazingira.
 
Nikitokwa jasho mwili huwasha, najikuna, kukosa uhuru na mara nyingine ninapokuwa sehemu yenye hewa iliyo na asili ya vumbi, napiga chafya mfululizo, kuwashwa uso na macho yanavimba na huwa nashindwa kupumua vizuri kwa sababu pua zinaziba,” anasema Evelyn.
Anasema anajitahidi kuhakikisha chumba anacholala
 
kinakuwa safi muda wote, lakini hali inakuwa ngumu akiwa katika vyombo vya usafiri kama daladala iliyojaza abiria kupita kiasi, kupita sehemu yenye harufu mbaya, au kutimuliwa vumbi barabarani.
Ushauri
Dk Fazel anasema ni vizuri watu wakazingatia na kufanya utafiti ili kuweza kugundua ni kitu gan
 
kinawasababishia mzio au kufika katika kituo cha afya kinachotoa huduma ya vipimo waweze kufanyiwa vipimo na kupata ushauri wa kitaalamu.
Na endapo mtu atatumia dawa zenye madini ya sulfer zikamletea madhara, anatakiwa awahi kumuona daktari ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…